Habari za Punde

Benki ya DTB Yakabidhi Bustani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Baada ya Kumaliza Ujenzi Wake Vuga.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DTB Ndg. Viju Cherian wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa bustani ya katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Vuga, kushoto Meya wa Manispa ya Zanzibar Ndg. Abdulrahaman Khatib Abdurahaman

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Mhe.Talib Ali na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DTB Tanzania Mr. Viju Cherian wakipiga makofi baada ya Uzinduzi na makabidhiano ya Bustani ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi iliofunguliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. Mhe. Riziki Pembe Juma. 
Mkuu wa Maoko wa Benki ya TDB Sylvester Bahati akizungumza baada ya uzinduzi huo wa bustani wakati wa makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Vuga Unguja.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.