Habari za Punde

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MITAMBO YA MKONGO WA TAIFA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (Wa tatu kulia), akiwaelekeza jambo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea mitambo ya Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa unaoendeshwa na TTCL Corporation.
Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (wa kwanza kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea sehemu ya mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano jijini Dar es Salaam inaoendeshwa na TTCL Corporation.Mtaalamu wa mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation (kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea mitambo ya Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa unaoendeshwa na TTCL Corporation.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge.
Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (katikati) akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kutembelea mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano jijini Dar es Salaam inaoendeshwa na TTCL Corporation.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.