Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe. Samia Suluhu Hassan Aanza Ziara Yake ya Siku Tano Mkoani Songwe Leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Lt. Mstaafu Chiku Galawa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Songwe tayari kwa ziara ya siku 5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Songwe tayari kwa ziara ya siku 5. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Lt. Mstaafu Chiku Galawa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Songwe tayari kwa ziara ya siku 5. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Songwe tayari kwa ziara ya siku 5.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) ​ 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Songwe tayari kwa ziara ya siku 5.
Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Lt. Mstaafu Chiku Galawa, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.
Akiwa mkoani Songwe, Makamu wa Rais atakagua na kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo ambapo atatembelea Wilaya Tatu za Mkoa huo ambazo ni Mbozi, Momba na Ileje. Makamu wa Rais ataanzia ziara yake katika Wilaya ya Mbozi ambapo miongoni mwa shughuli atakazofanya ni pamoja na kukagua na kufungua kituo cha Afya Nanyala, kusalimia wananchi katika eneo la mradi la Nanyala, kuweka jiwe la Msingi katika Mradi wa maji Iyula na kufanya Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Iyula.
Makamu wa Rais pia atatembelea Wilaya ya Momba ambapo atakagua na kuzindua kituo cha Afya Tunduma, atakagua shughuli za vikundi vya wajasiriamali Tunduma na kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wananchi wa Wilaya ya Momba.
Vilevile, Makamu wa Rais atatembelea Wilaya ya Ileje ambapo atapokea taarifa ya shughuli za uhifadhi wa mazingira na upandaji miti na kukagua shughuli za uhifadhi na  shamba la miti la Wakala wa Misitu Tanzania lilopo Katengele na baadae kufanya mkutano wa hadhara  katika kijiji cha Isoko ambapo atapata fursa ya kuzungumza na wananchi wa Ileje.
 Mhe. Makamu wa Rais atahitimisha ziara yake Mkoani Songwe tarehe 25, Julai 2018.

Imetolewa na;
Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai 21, 2018

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.