Habari za Punde

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan Aongoza Kikao Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.Yajadili Majina 19 ya Wagombe Uwakilishi Jimbo la Jangombe Zanzibar. .

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi 19 wanaowania kuteuliwa kugombea Nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar, baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Abdallah Maulid Diwani kufukuzwa Chama na nafasi hiyo kuwa wazi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutangaza Nafasi hiyo. Kujazwa kupitia Uchaguzi Mdogo.   
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluh Hassan, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar kuongoza Kikao cha Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, kujadili 
Majina ya Wagombea Nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Jangombe Zanzibar.  
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi, akitowa maelezo ya Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar uliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, Kilichoongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kujadili Majina ya 19 ya Wanachama wa CCM Waliojitokea kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea Jimbo la Jangombe Zanzibar katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, kulia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi. 

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakifuatilia maelezo wakati wa Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar kupitia majina ya Wagombea nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Jangombe Zanzibar.


MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Makamu 


wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Julai 9, 


mwaka 2018 ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa 


Zanzibar.
Makamu wa Rais Mhe. Samia ameongoza kikao hicho baada ya kupendekezwa 

na  wajumbe wa kikao kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Ibara ya 108 (4) ili aongoze kikao 


hicho kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Dk. Ali Mohamed  Shein aliyesafiri nje ya 


nchi kikazi.
Kikao hicho kimefanyika kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 7:30 mchana katika 

ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Kisiwanduzi Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilikuwa na ajenda moja ya kujadili kwa kina 

majina 19 ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kugombea nafasi ya 


uwakilishi katika jimbo la Jang’ombo Zanzibar.
Wanachama hao 19 walioomba nafasi hiyo na kupendekezwa katika ngazi za jimbo, wilaya 

na Mkoa, Kikao hicho kimeweka alama zinazostahiki kwa wagombea wote na kupendekeza 


kwa Kamati Kuu ya CCM Taifa ili irejeshe majina matatu au kama itakavyoona inafaa kwa 


ajili ya kura ya maoni kwa lengo la kumpata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera 


ya CCM katika Uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
Kikao hicho ni maalum kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2017, ibara 

ya109 (1) na 7(b).
Mchakato huo unafanyika kutokana na Jimbo la Jang’ombe kuwa wazi baada ya aliyekuwa 

Mwakilishi wa Jimbo hilo Abdalla Diwani  kufukuzwa uanachama wa CCM hivi 


karibuni  baada ya kukiuka maadili na miongozo ya Chama.

Imetolewa :-
Catherine Peter Nao.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
Idara ya Itikadi na Uenezi CCM- Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.