Habari za Punde

Mwenge wa Uhuru wawasili Pemba kuanza kukimbizwa Mkoa wa Kaskazini Pemba
 MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othaman mwenye jungle Hat, akimfahamisha jambo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, wakati walipokuwa wakisalimiana kabla ya kumkabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Uongozi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa, mara baada ya kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru kutoka Kisiwani Unguja.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MWENGE wa Uhuru ukiwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba Airport ukitokewa Mjini Magharibi Unguja, baada ya kukimbizwa na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 MAAFISA wadhamini kutoka Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na Afisha mdhani Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, Fatma Hamad Rajab katikati mwenye mtandio mweusi, wakishuhudia makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili kutoka kisiwani Unguja.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, akibadilishana mawazo na Kiongozi wa wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuri Kitaifa, Chales Francis Kabeho baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Pemba Airpot ukitokea Mjini Magharibi Unguja.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, akitoa nasaha zake kwa uongozi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika hafla ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru ulipowasili Kisiwani Pemba, kwa lengo la kukimbizwa kwa mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WAANDISHI wa habari kutoka Vyombo mbali mbali vya habari Zanzibar wakiwa wanafuatilia kwa karibu makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru ulipowasili Kisiwani Pemba, kutokea Mkoa wa Mjini Magharibi na kukabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MMOJA wa wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuru Kutoka mkoa wa kusini Pemba Issa Abass, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman, mara baada ya kuwasili kwa mwenge huo kutoka Mjini Magharibi.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MMOJA wa wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuru Kutoka mkoa wa kusini Pemba Issa Abass, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Sheikhan Mohamed, mara baada ya kuwasili kwa mwenge huo kutoka Mjini Magharibi.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 Kiongozi wa wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuri Kitaifa, Charles Francis Kabeho, akitoa shukurani zake kwa uongozi wa mkoa wa Mjini Magharibi kwa muda wote waokuwepo, baada ya kuwasili Kisiwnai Pemba kwa mwenge wa Uhuru na kuanza kukimbizwa Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, akimkabidhi taarifa mkoa wa Mjini Magharibi pamoja na wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuru, baada ya kuwasili Kisiwani pemba ukitokea Kisiwani Unguja.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othaman, mara baada ya kuwasili kutoka Unguja na kuanza kukimbizwa katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Omar Khamis Othaman, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali na Kuanza kuukimbiza katika maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo.(PICHA NA:ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.