Habari za Punde

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) latoa msaada wa dawa na vifaa vya tiba vyenye thamani zaidi ya Dola Milioni moja

  BAADHI ya Dawa na Vifaa Tiba vilivyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)  kwa Wizara ya Afya Zanzibar.
  MWAKILISHI wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tanzania (WHO) Dkt. Adiele Onyeze akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya  Dawa na Vifaa Tiba vilivyotolewa na Shirika la Afya Duniani  kwa Wizara ya Afya Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Ngalawa Bububu Mjini Zanzibar.
 NAIBU Waziri wa Affya Zanzibar Harus Said Suleiman pamoja na Mwakilishi wa  WHO Tanzania Dkt. Adiele Onyeze wakitiliana saini makabidhiano ya Dawa na Vifaa Tiba kwaajili ya Wizara ya Afya Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Ngalawa Bububu  Zanzibar. Dawa hizo zina thamani ya Us Dollars 1,164.635
 NAIBU Waziri wa Affya Zanzibar Harus Said Suleiman akibadilishana hati za makabidhiano ya Dawa na Vifaa Tiba na Mwakilishi wa WHO Tanzania Dkt. Adiele Onyeze katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Ngalawa Bububu Zanzibar.
 NAIBU Waziri wa Affya Zanzibar Harus Said Suleiman akionesha kifaa cha kuchunguzia maradhi ya EBOLA, ( katikati) ni Mwakilishi wa Tanzania (WHO) Tanzania Dkt. Adiele Onyeze, kushoto Mkurugenzi kinga Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed.
Picha na Abdalla Omar  Maelezo  - Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.