Habari za Punde

Usajili Kwa Wafanyabiashara Kutumia Mtandao "Online Regestration System" Zanzibar.


SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA MALI
ZANZIABAR - BPRA
TANGAZO

Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) inapenda kuwajuuilisha wafanyabiashara na wananchi kuwa imeanza rasmi kutumia mfumo wa usajili kwa kutumia mtandao Online Registration System’ (ORS) kuanzia tarehe 01/07/2018. Huduma zote zinazohusiana na usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Jumuiya za Kiraia (NGOs), Vyama vya Ushirika na Mashirika ya Serikali. Pia usajili wa Amana za Mali Zinazohamishika zinatolewa kupitia mifumo hiyo kwa anuani ifuatayo:-orsz.bpra.go.tz

Aidha taasisi zote zilizosajiliwa kabla ya matumizi ya mifumo ya usajili zinapaswa kuingiza taarifa zao kwenye mfumo wa usajili bila ya malipo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe ya kutumika mfumo huo.

Ili kuweza kutumia mfumo huo muombaji anapaswa awe na:-
1
.      Kitambulisho cha Mzanzibari Ukaazi ‘Zan ID’ au Kitambulisho cha Taifa National Identity Card’ kwa raia wa Tanzania.
2.     Kwa wageni awe na pasi ya kusafiria ‘Passport’
3.     Anuani ya barua pepe (email account).
Ada zote zinazohusiana na huduma hizi zitalipwa katika Benki yaWatu wa Zanzibar ‘The People’s Bank of Zanzibar’ (PBZ) ambapo taarifa zake zinapatikana kwenye mfumo huu.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya BPRA; www.bpra.go.tz,au www.orsz.bpra.go.tz
Imetolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA)
S.L.P 260, Zanzibar – Tanzania
Barua pepe: info@bpra.go.tz




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.