Habari za Punde

Waziri Kangi Lugola na Mhandisi Isaac Kamwelwe Watembelea Eneo la Ajali na Majeruhi wa Ajali Iliotokea Katika Eneo la Mlima Iwambi Jijini Mbeya.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimjulia hali mmoja wa majeruhi  aliyelazwa  katika Hospitali ya Rufaa Ifisi, ajali hiyo  iliyotokea hivi karibuni, katika eneo la Mlima Iwambi,jijini Mbeya
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac  Kamwelwe (kushoto),na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), wakimjulia hali mmoja wa majeruhi aliyelazwa katika Hospitali Teule ya  Mbalizi, ajali hiyo iliyotokea hivi karibuni, katika eneo la Mlima Iwambi,jijini Mbeya
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi katika eneo la Mlima Iwambi,jijini Mbeya, ambako hivi karibuni kumetokea ajali iliyosababisha vifo na majeruhi
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Dkt. Louis Chomboko, akitoa taarifa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola(kulia) na  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac  Kamwelwe (katikati) ,juu ya hali  za majeruhi wa ajali waliolazwa katika Hospitali ya  Teule Mbalizi, ajali hiyo  iliyotokea hivi karibuni katika eneo la Mlima Iwambi,jijini Mbeya
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisalimiana na watumishi wa afya baada ya kuwasili Hospitali ya Teule Mbalizi, kuwajulia hali majeruhi wa ajali iliyotokea katika eneo la Mlima Iwambi,jijini Mbeya.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.