Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Lee Nak-Yon wakati mgeni huyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kamabarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa Ziara ya siku tatu chini Tanzania
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Lee Nak- Yon baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa Ziara ya siku tatu nchini Tanzania
Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa na Rais wa Jamhuri ya Korea ,Le Nak Yon wakifurahia ngoma kwenye uwanja wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Juilai 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na.Mwandishi wa OWM.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempokea
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon ambaye amewasili
nchini leo saa 12:30 jioni (Jumamosi,
Julai 21, 2018) kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Kwenye uwanja wa ndege, Waziri Mkuu
huyo wa Jamhuri ya Korea alipokelewa pia na Waziri wa Mambo ya Nje, Dk.
Augustine Mahiga, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Isack
Kamwele, Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Eng. Stella Manyanya na viongozi wa mkoa wa Dar es
Salaam.
Waziri Mkuu Lee Nak-yon anatembelea
Tanzania ikiwa ni hatua ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi
hizi mbili. Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa nchi hiyo
kufanya ziara ya kiserikali tangu nchi hizo zianzishe mahusiano ya kidiplomasia
mwaka 1992.
Pia ameambatana na ujumbe wa maafisa
wa Serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa ambao watashiriki Kongamano la
Kibiashara baina ya Korea na Tanzania (Korea-Tanzania Business Forum) lililopangwa
kufanyika kesho kutwa (Jumatatu, Julai 23, 2018) kwenye hoteli ya Serena,
jijini Dar es Salaam.
Kesho (Jumapili, Julai 22, 2018), Waziri
Mkuu Lee Nak Yon atakuwa na mazungumzo rasmi ya kiserikali na mwenyeji wake
pamoja na viongozi kadhaa wa Serikali na pia kwa pamoja watashuhudia uwekaji
saini mkataba wa kuondoa hitaji la viza kwa watu wenye hati za kusafiria za
kidiplomasia na za utumishi (diplomatic and service passports).
Pia ataenda Ikulu kumsalimia Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, atatembelea
Makumbusho ya Taifa, Hospitali ya Mnazi Mmoja na kituo cha utunzaji taarifa cha
NIDA kilichopo Kibaha.
Anatarajiwa kuondoka nchini Jumatatu
jioni, Julai 23, 2018.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JULAI 21,
2018.
No comments:
Post a Comment