Habari za Punde

Bi. Zuwena Salum Said, Aliyekuwa Mkaazi wa Jengo Hilo Ahudhuria Uzinduzi wa Jumba la Treni Darajani Zanzibar.

Bi.Zuwena Salum Said akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mamhoud alipowasili katika viwanja vya Darajani kuhudhuria Sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Jumba la Treni Darajani Bi. Zuwena alikuwa mkaazi wa jengo hilo alikataa kuhama na kuchukuliwa busara na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub na kumuhamishia katika nyumba za Wazee Sebleni amekaa kwa muda mfupi na kuchukuliwa na Jamaa zake na kuishi katika mitaa ya Mkunazini Unguja.

Bi. Zuwena amepata ofa ya kukaa bure katika nyumba zilizo katika jengo hilo kwa maisha yake yote bila ya kulipia kodi.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akimsikiliza Bi. Zuwena Salum Said, baada ya kumsalimiana wakati akihudhuria hafla ya Uzinduzi wa Jumba la Treni Darajani.  
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud akisalimiana na kuzungumza na Bi.Zuwena Salum Said aliyekuwa mkaazi wa jengo Hilo akihuduria hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jengo la Treni baada ya kukamilika Ujenzi wake makubwa wa Maduka ya kisasa.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud akiwa na Bi Zuwena akimshindikiza kumpeleka katika sehemu ya kukaa kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya sherehe za Uzinduzi wa Jumba la Treni Darajani Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud akiwa na Bi Zuwena akimshindikiza kumpeleka katika sehemu ya kukaa kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya sherehe za Uzinduzi wa Jumba la Treni Darajani Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa Mstaaf wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kwa Sasa ni Msauri wa Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akiwa na Bi. Zuwena Salum Said wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kulizindua rasmin jengo hilo leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.