Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli Akutana na Kufanya Mazungumzo na Mgeni Wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kupita kwenye Gadi ya Heshma katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akiangalia kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya siku moja nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni, akimtambulisha kwa Viongozi wa Serikali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya siku moja nchini.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na wanahabari hawapo pichani mara baada ya kikao chake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari hawapo pichani mara baada ya kikao chake na Rais wa Uganda Yoweri Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kutoka kwenye chumba cha mkutano wa Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Uganda Yoweri , baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.