Habari za Punde

Sala ya Eid el Hajj ilivyosaliwa kitaifa Makunduchi


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hassan Khatib Hassan  wakati alipowasili katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo kabla ya  Swala ya Eid  el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo waislamu mbali mbali  walihudhuria,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Mashekhe wakati alipowasili katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja kabla ya  Swala ya Eid  el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo waislamu mbali mbali katika Mkoa huo  walihudhuria,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali na Mashekhe wa Mkoa wa Kusini Unguja  katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa  iliyoswaliwa leo  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja,ambapo Swala hiyo imeongozwa na Sheikh  Suleiman Haji Ibrahim,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018.
 Waislamu mbali mbali wa Mkoa wa Kusini Unguja  wakiwa katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa  iliyoswaliwa leo  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini,ambapo Sheikh  Suleiman Haji Ibrahim(hayupo pichani) aliongoza Swala hiyo,iliyohudhuriwa na Viongozi  wa Kitaifa akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018.
 Baadhi ya akinamama waliojumuika katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini  Unguja,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018. 
 Sheikh Abdalla Issa Makame (kulia) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja akisoma Khutba mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine pamoja na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja leo baada ya Swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika uwanja wa Jamhuri Makunduchi,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Swala ya Eid el Hajj wakisikiliza Khutba iliyosomwa na Sheikh Abdalla Issa Makame (hayupo pichani) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini,ambapo Viongozi wa Kitaifa walihudhuria katika  Swala hiyo iliyoswaliwa Kitaifa  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduzi Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018.
 Waislamu wakimsikiliza Sheikh Abdalla Issa Makame (hayupo pichani) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini  akisoma Khutba ya Swala ya Eid el Hajj, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine pamoja na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja leo baada ya Swala hiyo iliyoswaliwa katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine na Waislamu mbali mbali waliohudhuria katika Swala ya Eid el Hajj wakiitikia dua iliyoombwa na Sheikh Abubakar Ali Mohamed (wa pili kuilia) baada ya Swala hiyo iliyoswaliwa Kitaifa katika Mkoa wa Kusini Unguja   leo  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi, Wilaya ya Kusini,[Picha na Ikulu.] 22 Aug 2018. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.