MENEJA wa Redio Jamii Mkoani Ali Abass wa kwanza Kulia,
akisoma taarifa fupi ya Redio hiyo kwa watendaji wa UNESCO wakati walipofika
kuangalia mambo mbali mbali katika redio jamii Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WATENDAJI wa UNESCO Tanzania wakiongozwa na Meneja
wa Mradi wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari, Christopher Legal pamoja na
Afisa wa Kitengo cha mawasialiano na Habari UNESCO Tanzania Rose Nguwangwa,
wakiangalia utendaji kazi wa studio ya Redio Jamii Mkoani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
FUNDI mitambo wa Redio Jamii Mkoani Said Baraghashi,
akitoa maelezo kwa watendaji wa UNESCO Tanzania, wakati walipotembelea Studio
ya Redio hiyo katika ziara yao ya kuangalia mambo mbali mbali katika Radio za
Jamii Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
MAAFISA wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka
UNESCO Tanzania, wakiangalia mnara wa
kurushia matangazo wa Kituo cha Radio Jamii Mkoani, wakati walipofanya ziara
yao Kisiwani Pemba kutembelea Radio za Jamii.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MAAFISA wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari Kutoka
UNESCO Tanzania, wakizungumza na wasikilizaji wa Radio Jamii Mkoani huko Kisiwa
Panza, lengo ni kupata maoni ya wasikilizaji wa redio hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment