Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo
kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Paul Mamba Swea wakati wa
ziara hiyo
NA MWANDISHI WETU, MPWAPWA.
MKUU wa wilaya ya Mpwapwa mkoani
Dodoma Jabiri Shekimweri amesema wanalitumia zao la Korosho kujenga
uchumi,kuimarisha mapato yao sambamba na vyanzo vyengine vya Halmashauri
kutokana na kwamba bado ni zao jipya kwao.
Shekimweri aliyasema
hayo wakati akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini
waliofanya ziara ya kutembelea wilaya hiyo ambapo pia waliweza
kuwatembelea wakulima ikiwa ni mpango wao kupita kwenye maeneo mapya
yanayolima zao hilo kuwahamasisha wakulima ikiwemo shamba la mfano la
magereza wilayani Mpwapwa.
Alisema hilo linatokana na kwamba
agenda ya zao la Korosho ndio wanalisimamia kwa wigo mpana na
walikubaliana kwenye Halmashauri ikiwemo Baraza la madiwani ,Vikao vya
Kamati ya Ushauri ya wilaya hiyo (DCC) wakiwemo wadau mbalimbali kwamba
wajenge uchumi wa wilaya hiyo kwa kutumia zao la mkakati la Korosho.
Alisema
katika agenda ya zao hilo wilayani humo hakuna namna nyengine watapata
maendeleo kama hawatalichukua kama zaoi lao la uchumi na kuendelea
kuhimiza wananchi kujikita kwenye kilimo hicho kutokana na kuwa na faida
lukuki.
“Kwa kweli agenda hizi tatu ni kubwa kujenga uchumi
kupitia korosho,kuimarisha mapato ya wilaya yao kupitia Korosho na
vyanzo vyengine vya halmashauri kwa sababu ni zao jipya,kupitia korosho
mnyororo mrefu wanakwenda kutekeleza falsafa pana ya hapa kazi tu ya Mh
Rais wetu Dkt John Magufuli”Alisema DC Jabiri.
Alisema
uanzishwaji wa zao hilo unafaida nyingi ikiwemo kutengeneza ajira ya
kilimo cha biashara pia zao hilo litavutia viwanda vya ubanguaji korosho
na hivyo utajibu Tanzania ya viwanda.
“Kwani ukishakuwa na
uzalishaji mkubwa sekta nyengine zitakuja zikiwemo za usafirishaji
zitaamka na kuinua uchumi wa wilaya ya Mpwapwa,mkoa na Taifa kwa ujumla
“Alisema.
Aliongeza kwamba agenda ya pili ni kuanzisha mashamba
darasa ambapo vijana wa Boda boda wana ekari 12 ambazo wanalima korosho
lakini pia kuanzisha mashamba darasa ili watu waweze kujifunza ili
waweze kulima zao hilo.
Hata hivyo alisema mkakati tatu ni
kushawishi namna bora ya upatikanaji wa miche kwani wilayani hapo
walikuwa na vikundi saba vya uzalishaji ya miche kwa vitalu mwaka jana
walizalisha miche 480,000 huku miche 100,000 ikisomwa na maji baada ya
mvua kubwa kuonyesha.
Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa Mratibu
Magereza Joseph Mwita Sabayo aliishukuru bodi ya Korosho kwa
kuwatembelea kwenye shamba lao ambalo lilianzishwa mwaka 2009 likiwa
limetueliwa na wilaya hiyo kuwa shamba darasa ambalo wananchi walikuwa
wanajifunza kupitia shamba hilo.
Alisema hapo mwanzo mikorosho
ilikuwa ikionekana kulimwa mikoa ya kanda ya lakani baadae zao hilo
liliweza kuenea maeneo mbalimbali huku gereza hilo wakilima ekari elfu
hamsini na tisa wamejidhatiti kuhakikisha wanakuwa shamba la mfano
No comments:
Post a Comment