Habari za Punde

Gari ya Kampuni ya Ujenzi wa Mitaro Ikiwa Imepata Ajali Katika Moja ya Mitaro Inayojenga Katika Eneo la Lumumba Zanzibar.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Kichina inayojenga mitaro hilo wakilitizama Gari likiwa katika mtaro huo baada ya kutumbukia na kupinduka wakati likimwa kifusi katika zoezi la uchimbaji wa mitaro hiyo katika eneo la lumumba,ikiendelea na ujenzi huo wa Mitaro ya Maji Machafu katika maeneo mbalimbali ya maeneo ya Mitaa ya Mji wa Zanzibar ikiwa imeingia katika moja ya mitaro hiyo inayoendelea na ujenzi wake katika maeneo ya lumumba Unguja wakati ikimwa kifusi na kutumbukia katika mtaro huo. Katika ajali hiyo hakuna mtu aleyejeruhiwa.
Kijiko cha Kampuni ya Kichina inayojenga Mitaro ya Maji machafu katika maeneo mbalimbali Zanzibar ikilizuiya gari hilo la kubebea kifusi na michanga wakati lililopoingia katika mtaro huo unaojengwa katika eneo la lumumba Zanzibar. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.