Habari za Punde

Mwakilishi Mteuli Kupitia CCM Jimbo la Jang'ombe Ndg Ramadhan Hamza Chande Akabidhiwa Cheti Cha Ushindi.

AFISA wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Mjini Mwanapili Khamis Mohamed (kulia) akimkabidhi  Cheti cha udhibitisho wa Ushindi wa nafasi ya Uwakilishi   Mwakilishi mteule wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande (kushoto) , aliyekuwa Wakala wa Mgombea wa CCM katika Uchaguzi huo Rajab Uweje Yakoub (wa pili kushoto).
MWAKILISHI mteule wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande akionyesha Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa Uwakilishi kupitia Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo uliofanyika Jana.
Wakala wa Mgombea Uwakilishi wa CCM Ndugu Rajab Uweje Yakoub (wa pili kushoto) akisaini Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa Uwakilishi cha Mwakilishi mteule wa CCM Jimbo la Jang’ombe.NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MWAKILISHI mteule wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Jang'ombe Ndugu Ramadhan Hamza Chande leo amekabidhiwa rasmi Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo hilo.

Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Mjini iliyopo Maisara na kuudhuriwa na Viongozi na Wanatendaji wandamizi Tume hiyo na  CCM.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Cheti hicho Mwakilishi mteule huyo Ramadhan Hamza ameahidi kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kufuata miongozo na taratibu zote za kisheria kwa maslahi ya wananchi wote wa Jimbo hilo.   

Amewashukuru wananchi na wanachama wa CCM wa Jimbo hilo kwa kumpatia ridhaa yangu kuongoza Jimbo hilo kupitia  utaratibu halali wa kidemokrasia. 

"Nitawatumikia kwa uadilifu wananchi wote wa Jang’ombe bila ya ubaguzi wowote kwani naamini bila yenu nyinyi kuridhia kunipa nafasi hii nisingeweza kushinda katika mchakato huu wa kisiasa uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 tayari nishakabidhiwa muda wowote nitaanza kutekeleza mpango kazi wangu kwa lengo la kutekeleza ahadi nilizoahidi katika kampeni.”,ameeleza Chande.

Kwa upande wake aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Jang'ombe ambaye pia ni Afisa wa ZEC Wilaya ya Mjini Bi.Mwanapili Khamis Mohamed amemsisitiza kiongozi huyo kufanya kazi zake kwa majibu wa taratibu na kanuni za kisheria ili kutimiza matakwa ya wananchi waliomchagua. 

Mwakilishi huyo aliyeshinda nafasi hiyo jana kwa kura 6,581  sawa na asilimia 90.5 katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang'ombe uliofanyika kwa amani bila ya kujitokeza matukio ya uvunjifu wa sheria za Uchaguzi na nchi kwa ujumla. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.