Habari za Punde

Mwenyekiti wa Kamati ya TASAF Unguja Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mahmoud Atembelea Kituo Kipya cha Afya Kianga Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa TASAF Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Uratibu shughuli za Serikali Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Khalid Bakar (alievaa suti nyeusi) alipofanya ziara ya kutembelea kituo cha afya Kianga Wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya TASAF  Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib akizungumza na Wananchi wa Kianga (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kutembelea kituo cha Afya cha Kijiji hicho.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kianga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya TASAF Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib baada ya kutembelea ujenzi wa kituo chao kipya cha afya.
Muonekano wa Kituo kipya cha Afya cha kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja ambacho kiko katika hatua za mwisho kumalizika.Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir    - Maelezo.                  12-10-2018.
Mwenyekiti wa kamati  ya Uongozi wa TASSAF Unguja  
Ayoub Mohamed Mahmoud  amesema kumalizika kwa  kituo 
cha afya  Shehia ya Kianga  Wilaya ya Magharib “B” kitatoa 
huduma kwa wananchi wa maeneo ya shehia hiyo na 
majirani.

Akizungumza na wananchi wa shehia ya Kianga  alipokuwa 
akikagua kituo cha afya cha shehia hiyo na kuona jinsi 
kinavyoendelea na ujenzi wa mradi huo amesema ni juhudi 
za wananchi wa shehia ya Kianga wilaya ya Magharib A .

Alisema kituo hicho kitakapomalizika tayari watumishi 
wanaostahiki wataletwa wa kutosha  kwa kutoa huduma kwa 
wananchi wa Shehia hiyo kwa ajili ya kupata matibabu kwa 
lengo la kuondoshewa usumbufu .

“Kituo kitakapomalizika msiwe na wasiwasi tayari 
wafanyakazi watakuwepo kwa kufanya kazi hiyo na ufanisi 
zaidi ili kuona wananchi wanapata huduma hiyo kwa 
urahisi”.Alisema Mwenyekiti huyo ambaye pia ni 
Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Magharib.

Pia alisema mashirikiano ya Serikali zote mbili ikiwemo ya 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali 
ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa inaboresha Vituo vya Afya 
kwa kuwasogezea karibu na wanamoishi  ili  wananchi 
waweze kufaidika na huduma hiyo mjini na vijijini bila ya 
usumbufu.

Nae sheha wa Shehia ya Kianga Juma Issa Juma alisema 
wanashukuru  kupata mradi wa TASSAF  kwa kuwapatia 
 kituo hicho cha  Afya ambacho kitakapomalizika  tutafaidika 
kwa kupata huduma hii kwa urahisi zaidi.

Alisema wananchi wa Kianga watafaidika kwa asilimia mia 
moja kwani ugonjwa hauna muda maalum lakini kituo kipo 
hapa madaktari watakuwepo tutakuwa wenye kufaidika na 
matunda ya nchi yetu kwa kupitia viongozi wetu wa nchi.

Vile vile sambamba na hayo mwananchi wa shehia hiyo 
Subira Mohamed Jecha  amesema kwa sasa tumo furahani 
wananchi sote hasa  akinamama kwani kutatupunguzia 
masafa marefu ya kufatia huduma hiyo ya Afya  tukiwa na 
watoto au wajawazito kwani huduma hii tunaifata Mwera au 
Kizimbani.
Mwisho.
Imetolewa na idara ya Habari Maelezo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.