Habari za Punde

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Masauni Afanya Ziara Mkoani Arusha leo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tayari kuelekea jijini Arusha kwa ziara ya kikazi.Katikati ni Mkuu wa Kituo cha Polisi KIA, Mrakibu Msaidizi Abel Mgode na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi Zauda Mohamed.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiweka saini katika daftari la wageni baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tayari kwa ziara ya kikazi jijini Arusha.Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Mrakibu Msaidizi Zauda Mohamed na katikati ni Mkuu wa Kituo cha Polisi KIA,Mrakibu Msaidizi Abel Mgode.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.