Habari za Punde

TANESCO Yatoa Msaada wa Samani Shule Zinazozunguka Mradi wa Umeme wa Gesi Kinyerezi.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme, Mhandisi Raymond Seya, akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kibaga iliyo jirani na mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi jijini Dar es Salaam wakati alipofika kukabidhi samani za shule kwa shule zinazozunguka mradi huo Oktoba 12, 2018.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme nchini TANESCO, limekabidhi samani za shule kwa shule zinazozunguka mradi wa umeme Kinyerezi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni shukrani na kujenga ujirani mwema baina ya Shirika na wakazi wa eneo hilo.
Akizungumza Okatoba 12, 2018 jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kukabidhi samani hizo ambazo ni pamoja na meza na viti vya walimu, na madawati ya wananfunzi, Meneja wa Mradi, Mhandisi Stephenes S.A Mmanda alitaja shule zilizofaidika kuwa ni pamoja na Shule za msingi, Kibaga, Kinyerezi, Kijica, Zimbili, pamoja na shule za sekondari, Kinyerezi, Ulongoni, Ari na Kisungu.
Alisema, msada huo wa vifaa ni shukrani ya TANESCO kutokana na ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa na wakazi wa eneo hilo wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa umeme wa gesi Kinyerezi ambapo katika kipindi hicho, mradi ulizalisha ajiza zaidi ya 2000 wakiwemo mama ntilie ambao walipika vyakula kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi hao tangu Machi 2016 hadi hivi sasa.
 “Zaidi sana tulkisema ni vema tufanye kitu cha ziada kwa shule zinazozunguka, vifaa vyote vinavyokuja kwa ajili ya mradi vimefungwa kwa mbao na vingine kwa vyuma, tulisema hakuna haja ya kuharibu mbao wakati kuna wahitaji, hivyo tukaona tutengeneza  madawati,  viti na meza kama mnavyoona.” Alisisitiza Mhandisi Mmanda.
Alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza vilitolewa Julai 30, 2017, na shule zilizofaiodika ni pamoja na shule za msingi, Kinyerezi, Kibaga, Kijica na Zimbili.
Akieleza zaidi, Mhandisi Mmanda alitaja shule zilizofaidika awamu ya pili Novemba 2, 2017, kuwa ni pamoja na shukle za Sekondari, Kinyerezi, Ari na Kisungu.
"Sisi kama TANESCO tunaotekeelza mradi tumeona ni vema tuweze kushiriki kuhudumia jamii kwani msada huu utaleta hamasa na ni jukumu letu kushiriki kuona jamii pia inafaidika." Alisema Mhandisi Mmanda. 
Awali kabla ya hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vya awamu ya tatu Oktoba 12, 2018, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme, Mhandisi Raymond Seya, alitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa umeme Kinyerezi II na ule wa upanuzi Kinyerezi 1 ili kujionea maendeleo ya mradi huo ambapo alibainisha kuwa Mradi wa Kinyerezi II wa Megawati 240 umekamilika, na kwamba kazi iliyobaki ni ujenzi wa barabara na nyumba za wafanyakazi na kwamba tayari sehemu kubwa ya umeme unaozalishwa tayari umeingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
Aidha akielezea utekelezaji wa miradi yote miwili, Meneja Mradi Mhandisi Stephenes S.A Mmanda, alisema Mradi wa upanuzi Kinyerezi I uko katika hatua nzuri na umefikia asilimia 70, kwani miundombinu ya kusimika mashine imekamilika na sehemu kubwa ya vifaa tayari vimewasili.
“Mradi wa Kinyerezi unatoa Megawati 150, wakati huu wa upanuzi Kinyerezi I utazalisha Megawati 185 hivyo kutakuwa na jumla ya Megawati 335 zitakazizalishwa hapa.” Alisema Mhandisi Mmanmda na kuongeza Jumla ya Megawati 575 zitazalishwa kwenye miradi yote hii miwili ya Kinyerezi.

 Meneja wa Mradi, Mhandisi Stephenes S.A Mmanda(kulia), akipeana mikono na Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Mhe.Greyson Celestine, wakati wa kukabidhi vifaa hivyo.
  Meneja wa Mradi, Mhandisi Stephenes S.A Mmanda(kulia), akipeana mikono na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya msingi Kibaga wakati wa kukabidhi vifaa hivyo.
   Meneja wa Mradi, Mhandisi Stephenes S.A Mmanda(kulia), akipeana mikono na Mwalimu Mkuu  Shule ya Sekondari Ulongoni Bi.Sikitiko Salehe wakati wa kukabidhi vifaa hivyo.
Meneja wa Mradi, Mhandisi Stephenes S.A Mmanda, akizunguzma kwenye hafla hiyo.
Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akisalimiana na baadhi ya wanafunzi walioshuhudia utoaji wa msada hupo,
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme, Mhandisi Raymond Seya, akiwa ameketi na viongozi wanaosimamia mradi huo, wakati wa hafla ya kukabidhi samani hizo za shule.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.