Habari za Punde

Wadau wa Utalii Wakutana Kisiwani Pembe Kuzungumzia Utalii Kisiwani Pemba.

Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Khatib Juma Mjaja akizungumza katika kikao cha wadau wa utalii juu ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyoko Kisiwani Pemba, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa makumbusho Pemba
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akifungua kikao cha wadau wa Utalii Pemba, juu ya kuvitangaza vivutio mbali mbali vya kiutalii vilivyopo Kisiwani Pemba, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa makumbusho Chake Chake Pemba
VIONGOZI Mbali mbali wa Serikali na wadau wa Utalii Kisiwani Pemba, wakifuatilia kwa makini mada mbali mbali zinazoelezea vivutio vya utalii Pemba
AFISA Mdhamini wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Khatib Juma Mjaja akiwaonyesha wadau wa utalii Pemba, maeneo ya makamandume baada ya wadau hao wa utalii, kutembelea eneo la kihistoria la Mkamandume lililoko Pujini Chake Chake.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akipata maelezo juu ya chumba cha vitu vya asili, kutoka kwa msaidizi Mkuu wa Makumbusho ya Chake Chake  Salum  Seif mara baada ya wadau wa utalii kutembelea makumbusho ya chake chake
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na wadau wa utalii Pemba mara baada ya kumaliza ziara ya kutembele amoja ya kivutio cha utalii eneo la Mkamandume Wilaya ya Chake Chake(Picha na Abdi Suleiman- PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.