Habari za Punde

"Morogoro Marathon" Ilivyofana Baada ya Kufanyika Kwa Mara ya Kwanza Mkoani Morogoro.

Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathoni akiwemo Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Morogoro wakiwa wamejiapnga tayari kuanza mbio za Kilometa 21 zilizoanzia jirani na ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro.
 Kikundi cha Mazoezi cha Mzimuni Jogging Club wakiwa katika maandalizi ya kushiriki mbio hizo ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro.
 Kundi la Arusha Runners pia walikuwa ni washiriki wa tukio hilo .
Washiriki wa Mbio za Km 21 ,Morogoro Marathon wakipita katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro.
Wanariadha nguli ,Marko Joseph,Dickson Marwa,Faraja Lazaro ,Anthony Moya na Chacha Boy wakichuana vikali katika Mashindano mapya ya Morogoro Marathon yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa upande wa km 21.
Wanariadha Amina Mohamed na Rozalia Fabian kutoka klabu ya Jkt Arusha wakikimbia mbio za Kilometa 21 katika Mashindano mapya ya Morogoro Marathon yaliyofanyika mkoani Morogoro.
 Mshindi wa kwanza katika Mashindano Mapya ya Morogoro Marathon ,Amina Mohamed akimaliza mbio za Kilometa 21  kwa kutumia saa 1:21:47 akimshinda mpinzani wake ,Rozalia Fabian
 Mwanariadha Mkongwe Dickson Marwa akimaliza Mbio za Km 21 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
 Baadhi ya Washiriki mbalimbali wakimaliza Mbio hizo katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
 Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Mbio za Morogoro Marathoni.
 Baadhi ya Washiriki wa Mbio hizo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathoni .
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Kihanga akizungumza katika Mashindano hayo.
 Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa kwanza wa mbio za km 21 kwa wanawake Amina Mohamed zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
 Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa pili wa mbio za km 21 kwa wanawake Rozalia Fabian  zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
 Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa tatu  wa mbio za km 21 kwa wanawake Monica Nicolaus  zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
 Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa kwanza wa mbio za km 21 kwa wanaume ,Marko Joseph zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
 Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon ,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa  tatu  wa mbio za km 21 kwa wanaume  Faraja Lazaro zawadi ya king'amuzi cha DSTV.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Itete Sports Agency ambao ndio waandaaji wa Mbio za Morogoro Marathon ,Antipas Mgungusi akizungumza mara baada ya zawadi kukabidhiwa kwa washindi. 

Na Dixon Busagaga,Morogoro.

WANARIADHA Marko Joseph wa Singida na Amina Mohamed wa JKT –Arusha jana wamewek rekodi mpya baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa mbio za kilometa 21 kwa wananume na wanawake katika mashindano ya Mbio mpya za Morogoro Marathon 2018.
Joseph alifanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kutumia saa 1:05:50 akifuatiwa na mwanariadha Faraja Lazaro w JKT –A                rusha aliyemaliza mbio hizo zilizoanzia na kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri akituia saa 1:0:04.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na mwanariadha mkongwe Dickson Marwa aliyemaliza mbio hizo kwa kutumia saa 1:07:42 huku nafasi ya nne ikichukuliwa na mwanariadha Anthony Moya aliyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:07:42.

Kwa upande wa wanawake Amina Mohamed amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kutumia saa 1:21:47 akifuatiwa n Rozalia Fabiani liyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:23:59 huku Monica Nicolaus akishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 2:00:08.

Washindi wa Mbio za Kilometa tano wametangazwa Hashim Athuman (18:50:07) kwa upande wa wanaume huku kwa wanawake akishika nafasi ya kwanza Rosemary Mustapha  kutoka mjini Magharibi Zanzibar (23:41:66).

Nafasi ya pili kwa wanaume ni Mathayo Jeremia (Dar es Salaam), kwa wanawake niNeema Masoud wa JKT-Arusha huku nafas ya tatu kwa wanaume ikichukuliwa na Elias Maayunga na kwa wanawake ni Vaireth Kidosi.

Washindi katika mashindano hayo yanayoandaliwa na taasisi ya Itete Sports Agency walikabidhiwa zawadi  zao na Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe aliyekuwa mgeni rasmi ambaye pia alishiriki mbio za Kilometa tano.

Washindi kwa nafasi ya kwanza kwa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake wamejishindia fedha taslimu kiasi cha sh 400,000 na king’amuzi cha DSTVkutoka kampuni ya Mult choice ambayo ilikuwa moja wa wadhamini wa mbio hizo.

Washindi wa pili kwa mbio za km 21 wamejinyakulia kiasi cha Sh 250,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku washindi wa tatu wakijinyakulia kiasi cha Sh 100,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku washiriki  wengine wakiambulia zawadi za Medali .

Mwisho .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.