Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, Akiwaapisha Wajumbe Wapya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mjumbe Mpya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar, Dkt. Mohammed Sheif Khatib, Ikulu leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya kiapo ya Mjumbe Mpya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar Dkt. Mohammed Seif Khatib, baada ya kumaliza kula kiapo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Mohammed Seif Khatib, akimpongeza Mjumbe Mpya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar Dkt. Mohammed Sheikh Khatib, baada ya kumkabidhi Hati ya Kiapo, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mjumbe Mpya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar Ndg. Mbaraka Mohammed Abdulwakil, hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini Hati ya Kiapo ya Mjumbe Mpya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar Ndg. Mbaraka Mohammed Abdulwakil, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi hati ya kiapo Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar Ndg. Mbaraka Mohammed Abdulwakil, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  leo amewaapisha Wajumbe wapya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar.

Wajumbe walioapishwa katika hafla hiyo iliyofanyika  Ikulu mjini Zanzibar ni Dk. Mohammed Seif Khatib pamoja na Mbaraka Mohammed Abdulwakil.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Mawaziri, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Washauri wa Rais, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mzee Ali Haji.

Wengine ni Sheikh Hassan Othman Ngwali Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.