Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Amjulia Hali Mbunge wa Misungwi Mhe Charles Kitwanga.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, amtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Charles Kitwanga, alielazwa katika hospitali Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, akipata matibabu.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimpa pole, Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Mkunda ambaye anamuuguza mwanae, Tunu Kikula aliyelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa matibabu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa Kitengo cha Kusafisha Damu katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma wakati alipowajulia hali wagonjwa  hospitalini hapo, Januari 30, 2019.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.