Habari za Punde

Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Aweka Jiwe la Msingi Kituo Cha Afya Cha Kianga leo.

Jengo Jipya la Kituo cha Afya Kianga lililojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na kushirikiana na Wananchi wa Shehia ya Kianga Wilaya ya Magharibi A Unguja. limewekwa Jiwe la Msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Kinga  Wizara ya Afya Zanzibar.Dr. Fadhil Mohammed, wakati akitembelea jengo la Kituo cha Afya Kiangaa baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Kituo hicho akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Wilaya ya MagharibiA Unguja leo , akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika jengo la Kituo cha Afya Kiangaa baada ya kuliwekea Jiwe la Msingi leo akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Magharibi A Unguja, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Kinga wa Wizara ya Afya Dr. Fadhil Mohammed katikati anayefuatilia ni Daktari Dhamana wa Wilaya ya Magharib A Unguja Dr. Amina Hussein na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, , akielekea katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kupanda Mti wa Muembe katika eneo hilo la Kituo cha Afya Kiangaa baada ya uwekaji wa Jiwe la Msingi kulia Daktari Dhamana wa Wilaya ya Magharibi A Unguyja Dr, Amina Hussein na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akipanda Mti wa Muembe katika eneo la Kituo cha Afya Kiangaa baada ya kuweka Jiwe la Msingi, akiwa katika ziara yake katika Wilaya Magharibi A Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri, wakiwa katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Kiangaa Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ndg. Ladislous Mwamanga, akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Kiangaa , kilichojengwa na TASAF kwa kushirikiana na nguvu za Wananchi wa Shehia ya Kiangaa, wakati wa hafla hiyo iliofanyika leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wac Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TASAF .
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Abdallah Hassan Mitawi , akitowa Taarifa ya Kitaalam ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kianga wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Msingi la Kituo hicho leo. 

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mihayo Juma Nhnga, akizungumzia na kutoa shukrani kwa huduma hiyo ya Afya itawapunguziua Wananchi wa Kianga kufuata huduma ya Afya mbalim na makaazi yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Kiangaa Wilaya ya Magharibi A Unguja Mhe. Omar Haji Kheri, wakati wa hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar kuzungumza na Wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Shehia ya Kiangaa baada ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Afya Kiangaa leo wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Magharibi A Unguja.


Wananchi wa Shehia ya Kiangaa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Kiangaa leo, akiwa katika ziuara yake katika Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Wananchi wa Shehia ya Kiangaa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Kiangaa leo, akiwa katika ziuara yake katika Wilaya ya Magharibi A Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.