Habari za Punde

MAKAMBA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI WA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KUJADILI MASUALA YA MUUNGANO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongoza kikao kazi ngazi ya Mawaziri kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili masuala ya Muungano ikiwa ni kikao cha utangulizi kabla ya kikao cha Kamati ya Pamoja kitakachoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kikao hicho kimehudhiriwa pia na Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu wa Tanzania Bara na Zanzibar
Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akichangia katika kikao kazi cha Mawaziri wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kujadili masuala ya Muungano. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu Bunge Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki.

Sehemu ya Wajumbe wa kikao hicho ambao ni Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakifuatilia kikao hicho, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.