MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano |
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Rahma Msofe akizungumza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa |
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza katika halfa hiyo |
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu akizungumza katika halfa hiyo |
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo akizungumza katika halfa hiyo
Afisa Elimu Taaluma Jiji la Tanga akizungumza katima hafla hiyo |
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikanjuni Kaana Erasto akitoa taarifa ya shule hiyo |
Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo
Sehemu ya walimu wa shule hiyo wakifuatilia halfa hiyo ya
makabidhiano
Sehemu ya walimu wa shule hiyo wakifuatilia halfa hiyo ya
makabidhiano
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo kulia akiamkaribisha Mkuu wa
wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja
vya shule ya Sekondari Mikanjuni
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kiwa kwenye picha ya
pamoja mara baada ya kamabidhiano hayo
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akiwaongoza viongozi mbalimbali
wakati walipotembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya
Sekondari Mikanjuni
Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakifuatilia hotuba ya mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya ya Tanga
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akiagana na watumishi
wa mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) mara baada ya kumalizika kwa halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala
wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
Sehemu ya Kokoto zilizokabidhiwa
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akitokea nondo 60 kwa
ajili ya ujenzi
kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi
wa Mazingira
Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Rahma Msofe kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
imekabidhiwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya milioni 10 kwa ajili
ya kumalizia ujenzi wa madarasa kwenye shule ya sekondari Mikanjuni
ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali kuondosha
changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Halfa ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye shule hapa baina ya
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Rahma Msofe na Mkuu wa wilaya
ya Tanga Thobias Mwilapwa wakiwemo Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi
Geofrey Hilly na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim.
Vifaa vilivyokabidhiwa shuleni hapo kwa ajili ya kumalizia
madarasa matatu ni pamoja na saruji mifuko 100, nondo 60, shehena za
kokoto, mchanga, mbao, waya na vifaa vingine vyot ambavyo vitasaidia
ujenzi huo ili kutoa fursa wanafunzi kupata fursa ya kusoma bila
kuwepo kwa vikwazo vyovyote.
Akizungumza mara baada ya
kutokea msaada huo wa vifaa hivyo vya ujenzi Mkuu wa wilaya ya Tanga
Thobias Mwilapwa alipongeza juhudi ambazo zimefanywa na mamlaka hiyo
kwa kusaidia kuondosha changamoto za elimu kwenye shule hiyo.
Mwilapwa alisema juhudi ambazo zimefanywa na mamlaka hiyo
zinapaswa kuungwa mkono na mashirika ya Umma na makampuni binafsi
kuhakikisha yanachangia masuala ya elimu ili kuunga mkono juhudi za
serikali katika kukabiliana na uhaba wa madarasa.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema serikali inakabiliwa na changamoto kubwa hasa
katika sera yake ya elimu bure kutokana na idadi ya wanafunzi
wanaofaulu toka darasa la saba kwenda kidato cha kwanza kuongezeka
siku hadi siku na kupelekea uhaba wa vyumba vya madarasa.
Alisema mamlaka hiyo mbali na jitihada za kuimarisha huduma ya maji
nam usafi wa mazingira Jijini Tanga pia imechukua dhamana ya
kuimarisha miundombinu ya shule hiyo ambayo inauhitaji wa madarasa
kutokana na ongezeko la wananfunzi.
Awali akizungumza
katika halfa hiyo ya makabidhiano Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka
hiyo Rahma Msofe alisema kilichofanywa na Mamlaka hiyo ni sehemu ya
kuchangiaji wa huduma za kijamii ili kumuunga mkono Rais Magufuli
katika harakati zake za kuiboresha elimu.
Msofe alisema
vifaa vilivyotolewa shuleni hapo kwa ajili ya kumaliziamadarasa matatu
ni pamoja na saruji mifuko 100, nondo 60, shehena za kokoto, mchanga,
mbao,waya na vifaa vingine vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni
10.
“Malengo yetu si kuhudumia sekta ya maji tu bali
tutaendelea kujikita katika kusaidia huduma za kijamii pale
tutakapoona upo ulazima wa kufanya hivyo bila ya kuathiri utendaji wa
kazi zetu”Alisema Msofe.
Awali akisoma taariafa fupi
mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Shule hiyo Kaana Erasto alisema shule
hiyo iliyo na wanafunzi 1319 inauhitaji wa madarasa 33 huku yaliyopo
24 ambapo kunaupungufu wa vyumba 9 ili kutoa fursa kwa wananfunzi
kupata sehemu ya kujisomea.
Alisema jitihada za wadau
zimeanza na tayari ujenzi wa vyumba vitatu kati ya tisa umekwisha anza
na majengo yapo katika hatua za mwisho ili kuweza kukabiliana na uhaba
huo na kutoa fursa kwa wanafunzi ambao wamekosa mahala pa
kujisomea.
Erasto alisema wanafunzi waliopata nafasi ya
kujiunga na shule hiyo kidato cha kwanza mwaka 2019 ni 405 huku 150
ndio waliopo madarasani ambapo wanafunzi 255 wakikosa mahala ma
kujisomea na kupelekea wahisani kujitolea katika ujenzi wa
madarasa.
No comments:
Post a Comment