Habari za Punde

Vijana wa Majukwaa ya Vijana Mkoani Arusha Wametakiwa Kubuni Teknolojia za Viwandani.

Baadhi ya Vijana kutoka majukwaa ya vijana Wilaya ya Arusha wakiangalia Mashine zilizotengenezwa na Wabunifu wazawa katika karakana za SIDO mkoa wa Arusha ,ziara iliyoratibiwa na shirika lisilokua la kiserikali la INFOY la jijini hapa.
Vijana wakitembelea viwanda vidogo vidogo kwenye eneo la SIDO.
Mratibu wa Shirika la INFOY Laurent Sabuni akifafanua jambo katika Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyofanyika SIDO Mkoa wa Arusha.
Meneja wa SIDO mkoa wa Arusha Linah Nchimbi akitoa mada kwa vijana kutoka majukwaa ya vijana wilaya ya Arusha waliotembelea makao makuu ya SIDO mkoa wa Arusha kujifunza mambo mbalimbali
 Vijana wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali kwenye ziara hiyo

Na.Ahmed Mahmoud,Arusha.
Vijana nchini wametakiwa kubuni teknolojia Zitakazowasaidia wajasiriamali walioko kwenye viwanda vidogo vidogo ili waweze kuuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa bora zinazohimili ushindani wa soko .

Hayo yameelezwa na Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda la Sido mkoani Arusha Linah Nchimbi  alipotembelewa na Vijana kutoka Majukwaa  ya Vijana yaliyoandaliwa na shirika la INFOY ambapo amewataka vijana wa kitanzania kubuni teknolojia badala ya kuwa tegemezi kwa kutumia teknolojia kutoka mataifa ya nje jambo ambalo linawanufaisha kuliko wao.

Nchimbi alisema kuwa Sido inatoa fursa kwa vijana kufika na kutumia ubunifu wao ambao unaweza kubadilishwa na kuingia kwenye mfumo wa kibiashara hivyo kuwanufaisha.

Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali La INFOY ,Bw.Laurent Sabuni aliyefanya ziara SIDO kuangalia teknolojia zilizobuniwa na wazawa huku  akiongozana na vijana kutoka katika majukwaa ya Vijana katika Wilaya ya Arusha amesema kuwa vijana wanapaswa kuwa wabunifu Na kubuni teknolojia ambazo zutasaidia taifa kusonga mbele kuelekea uchumi wa viwanda..

Sabuni alisema kuwa ziara hiyo inalenga kuhamasisha vijana kuongeza hamasa ya kushiriki katika uchumi wa viwanda kwa kutumia ubunifu na fursa zinazowazunguka

“Nchi yoyote haiwezi kuendelea kama hakuna ubunifu wa teknolojia na bidhaa mbalimbali ambazo nchi inaweza kuviuza katika masoko ya nje na kuleta faida” Alisema Sabuni

Johnson Joseph Mmoja kati ya vijana wameeleza kuwa suala la ubunifu kwa vijana linapaswa kuhimizwa na  kuhakikisha linaungwa mkono na wadau wa maendeleo kwa kutenga maeneo ya uzalishaji..

Alisema kuwa kwa sasa wameanza kujifunza kuanzisha miradi mbalimbali itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini ikiwemo ufugaji kuku,na usindikaji wa bidhaa za nafaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.