Habari za Punde

Ifahamu Zaidi Kampeni ya Tokomeza Zero ya Wilaya ya Kisarawe Pwani.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akiwa anazindua kampeni ya Tokomeza Zero.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo (wa pili kutoka kushoto) akipata maelekezo katika  moja ya mahabara wilayani Kisarawe
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwigelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi katika mahafali ya kidato cha nne.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo (Kulia) akigawa vifaa vya  shule ikiwa ni sehemu ya kampeni ya   Tokomeza Zero Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akiwa picha ya pamoja na wanafunzi wa shule yaMakurunge
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi katika mahafali ya Darasa la Saba.


Tokomeza zero Kisarawe ni kampeni maalum kwa ajili ya kuongeza ufaulu na kuondoa kabisa zero Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani. Changamoto wanazopitia walimu na wanafunzi ni nyingi.  Elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo wana kisarawe wameona  ni vyema  kuwekeza katika Elimu

"Ukimsaidia mtoto akaweza kupata elimu unakuwa umeweza kusaidia Tanzania nzima,na mimi kuanzia sasa nataka tuanze  na kidato cha nne na sita tufute hizo zero na zisiwepo kabisa. Katika kuhakikisha hii linatimia kuna mambo mengi ambayo tutafanya kwa kushirikiana na wadau wote wa elimu nchini ." Alisema Mhe. Jokate Mwegelo

TUMEFANYA 
Mwaka jana kampeni hii ya tokomeza Zero  ilifanyika kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwa kuongeza ufaulu ikiwa ni kupunguza zero kutokea 455 mpaka 259 na kuondoa zero kabisa kwa kidato cha sita.  

Kwa kuona hili Mhesimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alizindua Kampeni dada ijulikanayo kama Tokomeza Zero Kisarawe ikijumuisha wanafunzi kuwekwa kwenye kambi kwa ajili ya mafunzo maalum, uboreshwaji wa miundo mbinu mashuleni na  Elimu na kozi kwa walimu ili kuinua kiwango cha Elimu Wilaya ya Kisarawe

Utafiti unaonyesha wanafunzi wengi wa kisarawe hutembea umbali mrefu sana kwenda shule (Zaidi ya km 15 kwenda pekee) hali inayofanya wanafunzi kufika shuleni wakiwa wamechoka, mtoto wa kike ambaye atahitajika kufanya usafi nyumbani kisha aende shule kwa kutembea huchoka zaidi.

Miundo mbinu ya shule  ni changamoto na hata idadi za shule Wilayani ni chache kwa kulitambua hilo kuna ushirikishwaji wa wadau wa Elimu ili kuwezesha ujenzi wa shule kwa ajili ya wana Kisarawe na mkazo unawekwa zaidi ili kufanikisha kampeni ya Tokomeza Zero"Wanafunzi wote wa Kisarawe wa kidato cha nne na cha sita watapata mafunzo ya ziada ili kujiandaa na mitihani yao ya taifa, ili kuwaepusha na kazi za kila mara wanafunzi hawa watakuwa kwenye kambi maaum kwa muda miezi miwili kabla ya muda wa mitihani yao ya taifa." Alisema Mhe. Jokate Mwegelo 

Sambamba na hilo walimu wanapatiwa mahitaji yote muhimu ili kufanikisha zoezi lao la ufundishaji na pia kuboresha miundo mbinu ya shule ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi na walimu.

Katika kufanikisha kampeni hii inaenda sawa imeandaliwa Dinner Gala tarehe  30/03/2019 Ukumbi wa Mlimani City, katika jitihada za kukusanya fedha ambazo zitatumika katika ujenzi ya mabweni, shule hiyo itakuwa na madarasa ya kutosha, maktaba pamoja na maabara za kisasa. Shule hiyo itakuwa ya kwanza ya aina yake Kisarawe na kama mdau wa Elimu unaweza kushiriki kwa kuchangia Tsh 100,000  au kununua meza moja kwa shilling million moja . 

Fedha zote hizi zitaelekezwa katika ujenzi wa shule hiyo ya kwanza ya aina yake yenye lengo la kuwa shule ya mfano ambapo shule zitakazofuatia zitaundwa kwa mfano huo.

Unaweza kushiriki kwa kuwasiliana nasi kwa namba hii ili kupata ticket yako 0677062070 au 0656132676

Asanteni


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.