Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar IkiendeleaKatima Viwanja Mbalimbali Unguja na Pemba

Na Hawa A Ally -Zanzibar
MICHUANO ya ligi kuu ya Zanzibar imeendelea kutimua vumbi  hapo jana katika viwanja mbalimbali vya hapa Visiwani Zanzibar
Katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba  majira ya saa kumi alasiri timu ya Jamuhuri imebuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya timu ya  Chipuki, kwa matokea hayo timu ya jamuhuri imefanikiwa kufikisha alama 30 na kujiweka katika nafasi ya 12 , huku chipukizi  nayo  ikibaki na alama 31  na kushikilia nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi hiyo.
Wakati katika Uwanja huo huo wa Gombani majira ya saa nane mchana timu ya Selem View imetoshana ngumu na timu ya Opec kwa kutoka sare isiyo na magoli , kwa matokeo hayo timu ya Opec imefikisha alama  23 ikiwa katika nafasi ya 16 huku selem View nao wakiwa na alama 28 wakiwa katika nafasi ya 13
Kwa upande wa Viwanja vya KIsiwani Unguja  ambapo ilipigwa michezo mitatu katika uwanja wa Amaan majira ya saa nane mchana  Timu ya Mafunzo imefanikiwa kuwashambulia maafande wenzao wa KVZ kwa kuwachapa bao 1-0 kwa matokeo hayoa Mafunzo imefanikiwa kufikisha alama 65 ikiwa nafasi ya 5,  huku maafande wa KVZ  wakiwa vinara wa ligi hiyo kwa alama zao 70.
Majira ya saa kumi Alasiri katika uwanja huo huo wa Amaan timu ya Mlandege nayo imewapa raha mashabiki wake kwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya timu ya  maafande wa Zimamoto kwa matokeo hayo maafande wa zimamoto wameendelea kubaki katika nafasi ya tatu katika msimo wa ligi hiyo wakiwa na alama 66 huku Mlandege wenyewe wakifikisha alama 63 wakiwa katika nafasi ya 6
Katika Uwanja wa Mau ze dong  Timu ya Jang’ombe boys nayo imefanikiwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya maafande wa JKU,  kwa matokeo hayo waliyoyapata Jang’ombe boys wamefanikiwa kufikisha alama 49 na kuwa katika nafasi ya 8 huku maafande wa JKU wenyewe wakiwa katika nafasi ya  pili  na alama zake 67.
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa kupigwa Michezomiwili ambapo katika Uwanja wa Mau majira ya saa kumi timu ya polisi itashuka Dimbani kuumana na  timu ya Chuoni, huku majira ya saa kumi katika Uwanja wa Amaan Timu ya Malindi itavaana na KMKM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.