Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama  (mwenye blauzi nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako.
Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia michango wa Wabunge wakati wa kujadili Hoja ya Mhe.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Mb) kuhusu mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/ 2020 Bungeni Dodoma Aprili 09, 2019.
 Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia michango wa Wabunge wakati wa kujadili Hoja ya Mhe.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Mb) kuhusu mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi yake kwa Mwaka wa FEdha 2019/ 2020 Bungeni Dodoma
 Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia michango wa Wabunge mapema hii leo Bungeni Dodoma, katikati ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi. Maimuna Tarishi, na mwenye tai nyekundu ni Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe wakati wa Bunge Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto) pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile (mwenye tai ya blue) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Andrew Massawe (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) mwenye tai nyekundu na Bi. Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu) nje ya Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu wakiteta jambo mara baada ya kuhairishwa kwa vikao vya bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma Aprili 09, 2019, kulia ni Bw. Andrew Massawe anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na kushoto ni Bi. Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu)
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.