Habari za Punde

Ujenzi wa Daraja katika Eneo la Barabara ya Fuoni Kibonde Mzungu Ukiwa Katika Hatua ya Mwisho ya Ujenzi Huo.

Muenekona wa Daraja la barabara ya Kibonde Mzungu likiwa la njia nne likiendelea na ujenzi wake katika hatua ya mwisho kumalizia ujenzi huo, eneo hilo lilikuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo wakati wa mvua za masika hujaa maji hadi kulifunika daraja hilo, kwa sasa kero hiyo imekuwa mwisho na kupitika kwa wakati wote wa mvua na kiangazi baada ya kukamilika ujenzi huo.
Ujenzi ukuendelea katika hatua za mwisho kumalizia Daraja la Kibonde Mzungu Barabara ya Fuoni ujenzi huo unaofanywa na kampuni ya ujenzi ya Mecco. 
Muonekano wa barabara ya Mwanakwerekwe ikitowa huduma kwa wananchi na vyombo vya moto , barabara hiyo itaungana na daraja la kibonde mzungu Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.