Habari za Punde

WAZIRI MHAGAMA AWAASA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJ

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Machifu wa Tamaduni za Asili na wakazi wa Ichenjeziya alipotembelea eneo kujionea chazo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Mkoani Songwe. (Kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, (Kulia) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akieleza jambo kwa Machifu wa Tamaduni za Asili na wakazi wa Ichenjeziya alipotembelea eneo kujionea chazo cha maji asilia Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja wa Machifu wa Tamaduni za Asili kuhusu chanzo cha maji cha Ichenjeziya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipanda mche wa mti karibu na chanzo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe.
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akipanda mche wa mti karibu na chanzo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akicheza pamoja na wanakwaya wa JKT Mlale alipofanya ziara ya kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 katika uwanja wa Kimondo, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde wakati wakiangalia kikundi cha Ngoma Asili (hakipo pichani) walipotembelea uwanja wa Kimondo kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiangalia Vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 (hawapo pichani) alipotembelea uwanja wa Kimondo kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Songwe. (Kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akieleza jambo kwa Viongozi mbalimbali walihudhuria uwanjani hapo kujionea maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Vijana wa Halaiki wakitengeneza umbo la Mlima Kilimanjaro kuashiria kupandisha Bendera ya Taifa katika mlima Kilimanjaro wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipotembea kukagua maandalizi hayo.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Na; OWM (KVAU), SONGWE
Wananchi waaswa kutunza rasimali mbalimbali katika mazingira yao na kuyapenda ili kuepuka kuathiri na kuharibu mazigira yaliyopo.
Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Ichenjeziya alipotembelea eneo hilo lenye chanzo cha maji ya asili na kupanda mche wa mti ikiwa ni siku ya Kitaifa ya upandaji miti.
Waziri Mhagama alieleza kuwa Nchi yetu imeamua kutumia uchumi wa viwanda ili kutekeleza azma ya Serikali kuelekea uchumi wa pato la kati, hivyo hata upandaji miti na maliasili ya misitu inaendana na uchumi wa viwanda,” alieleza Mhagama.
Aliongeza kuwa kuelekea kwenye Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019, ni vyema wananchi wakashiriki kauli mbiu ya upandaji miti ambayo inaendana na kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru isemayo “Maji ni Haki ya kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”.
“Wanaichenjeziya mnatakiwa kuweka historia kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu kwa kupanda miti kwenye vyanzo vya Maji ili kupata maji safi na salama,” alisema Mhagama
Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa kila mwananchi kuhakikisha anakuwa msimamzi wa mazingira na anatunza vyanzo vya maji kwa kufuata sheria na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anafikiwa na maji safi na salama kama haki ya msingi.
Hata hivyo Mhe. Mhagama alitumia pia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wa Songwe na Mikoa ya jirani kushiriki kwa wingi katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazozinduliwa Aprili 2, 2019 katika Uwanja wa Kimondo uliopo Kata ya Forest, Wilayani Mbozi.
“Hii ni nafasi ya kipekee kwa wananchi na ni siku ya kuhamasishana kwa vijana kwa kujitathimini na kutambua mchango wa Baba wa Taifa na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibari katika kujenga Taifa,” alisema mhagama
Naye Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume alisema kuwa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ni siku muhimu sana kwa wananchi kutambua historia ya Tanzania Bara na Zanzibar iliyopelekea Taifa katika mwanga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.