Habari za Punde

BRELA Watumia Maonesho ya Saba ya Kimataifa ya Biashara Jijini Tanga Kufanya Usajili wa Papo Kwa Papo.

Msajili Msaidizi kutoka kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) Suzana Senso akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Mwakidila ambao walitembelea Banda leo lililopo eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya saba ya Biashara ya Kimataifa
Msajili Msaidizi kutoka kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) Suzana Senso kushoto akiwa na kikundi cha Strong Women Group cha watu sita wakiwa wamepata cheti chao cha usajili cha jina la Biashara kwenye maonyesho ya Tanga Trade Fair 2019
Msajili Msaidizi kutoka kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) Suzana Senso kushoto akiwa na kikundi cha Strong Women Group cha watu sita wakiwa wamepata cheti chao cha usajili cha jina la Biashara kwenye maonyesho ya Tanga Trade Fair 2019

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) umesema kwamba wameamua kushiriki maonyesho ya saba ya Biashara ya Kimataifa mkoani Tanga ili waweze kufanya usajili wa papo kwa papo majina ya biashara.

Hayo yalisemwa leo na Msajili Msaidizi kutoka kitengo cha Ubunifu wa Wakala huo Suzana Senso wakati akizungumza na vyombo vya habari mjini hapa kuhusu uwepo wao kwenye maonyesho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.

Alisema baada ya kupata mwaliko kutoka TCCIA na hivyo kushiriki kwenye maonyesha hayo watakuwa wakitoa huduma za usajili wa makapuni, majina ya biashara na nembo za biashara

“Kwa kweli niwaambie wakazi wa mkoa huu wa Tanga na mikoa ya jirani wachangamkie fursa hii ya kuweza kutumia muda huu kuweza kusajili majina ya biashara zao, makampuni na nembo lakini pia leseni daraja A lililokuwa linasajiliwa Wizara limerudishwa kwetu na hivyo pia wanasajili iwapo walengwa watakidhi vigezo vilivyowekwa “Alisema

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kusajili ili kuweza kusajili kampuni lakini lazima vigezo na masharti husika vinavyohitajika kwenye upatikanaji wa leseni hiyo lazima uzingatiwe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.