Habari za Punde

PSSSF Yalipa Malimbikizo ya Mafao Zaidi ya Shilingi Bilioni 880 Kwa Wastaafu Elfu Kumi Nchini

NA K-VIS BLOG, DODOMA

ZAIDI ya Shilingi bilioni 880 zimetumika kulipa malimbikizo ya mafao ya wastaafu takriban elfu kumi (10000), wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF), Meneja Kiongozi, Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma leo Mei 29, 2019.

“Dhamira ya Mfuko ni kuhakikisha kuwa wanachama wake wanalipwa mafao yao kwa wakati na kwa hakika tutaendelea kutoa huduma bora kwa wastaafu na wanachama wetu.” Alisema Meneja huyo.
Alisema, wastaafu wote wanapaswa kuhakikiwa taarifa zao kama ambavyo matangazo yamekuwa yakielekeza
“Hadi kufikia Aprili 30, 2019 jumla ya wastaafu waliojitokeza kuhakikiwa ni 113,962, huku wastaafu wengine 10, 509 wakiwa bado hawajaripoti kwenye ofisi zetu ili kuhakikiwa taarifa zao,” Alifafanua Bi. Eunice Chiume na kuongeza
“Nitoe wito kwa wastaafu wote ambao bado hawajahakikiwa kufika kwwenye ofisi zilizo karibu naye ili ahakikiwe taarifa zake.” Alisema.

Meneja huyo Kiongozi, Uhusiano alibainisha kuwa had hivi sasa, Mfuko una jumla ya wastaafu 124,000 na wanachama 763,000 na kuwahakikishia kuwa Watumishi wa PSSSF wamejipanga kutoa huduma bora kwa wastaafu na wanachama wa Mfuko huo katika ofisi zote za Mfuko zilizo Tanzania bara na Visiwani.“Niwatoe hofu wastaafu, zoezi hili la uhakiki ni endelevu na kwamba Wanachama wanaweza kuwasiliana na Mfuko kupitia namba 0800 110 055, 0800 780 060 na 0800 110 040 (namba hizi ni bure). Pia wanaweza tuma ujumbe mfupi kwa namba 0735 117 773 na 0736 117 773 “PSSSF inaendelea kuunga mkono ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuwekeza kwenye viwanda kikiwemo kiwanda cha kuzalisha viatu cha Karanga kilichoko mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kinachoendeshwa kwa ubia kati ya Mfuko na Jeshi la Magereza.
Meneja  Kiongozi, Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bi. Eunice Chiume akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Mei 29, 2019. Amesema takriban wastaafu 10,000 kote nchini wamelipwa malimbikizo ya mafao yao.
Meneja  Kiongozi, Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bi. Eunice Chiume (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Mei 29, 2019. Amesema takriban wastaafu 10,000 kote nchini wamelipwa malimbikizo ya mafao yao. Kulia kwake ni Afisa Uhusianio Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi. (PICHA NA MAELEZO).


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.