Habari za Punde

Wananchi Washiriki Katika Maziko wa Mchezaji wa Zamani na Afrika Kids na Mwenyekiti wa CCM Wilaya yac Amani Kichama Unguja Yaliofanyika Katika Kijiji cha Jumbi Wilaya ya Kati Unguja.

Naibu Khadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali akiongoza Sala ya Kuusalia Mwili wa Marehemu Abdi Ali Mzee (Mrope) Sala iliofanyika Msikiti wa Kwa Boko Kidongochekundu Zanzibar baada t ya Sala ya Adhuhuri na kuzikwa katika makaburi ya Jumbi Wilaya ya Kati Unguja 
Mamia ya Wananchi Kisiwani Zanzibar wajumuika kuusalia mwili wa Marehemu Abdi Ali Mzee (Mrope) sala iliyofanyika Msikiti wa Kwa Boko Kidongochekundu Zanzibaer na kuzikwa katika makaburi ya Jumbi Wilaya ya Kati Unguja jana 26-5-2019. Kiongozi wa CCM Wilaya ya Amani Kichama akisoma wasifu wa Marehemu Abdi Ali Mzee (Mrope) baada ya kumalizika hafla hiyo ya maziko yaliofanyika katika makaburi ya Jumbi Wilaya ya Kati Unguja jana 26-5-2019.
Mwakilishi wa Famili ya Marehemu Abdi Ali Mzee (Mrope) akitowa neno la shukrani kwa Wananchi  kwa ushirikiano wao katika kufaniukisha shughuli za maziko ya ndugu yao, tokea kuunguza hadi kufikia hatua hii ya maziko hii leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.