Habari za Punde

Mnapaswa Kudumisha Nidhamu ya Matumizi ya Fedha Baada ya Kustaafu - Pinda.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda akizungumza na baadhi ya wastaafu wa Ofisi ya Wazir Mkuu walipomtembelea nyambani kwake eneo la Zuzu Jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu juu ya maandalzi ya kustaafu.Ziara hiyo ilifanyiki ikiwa ni sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea Juni 20, 2019. 
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi sehemu ya mimea ya zabibu aliyolima katika shamba lake la hekari 10 kwa ajili biashara wakati wa ziara ya watumishi wa ofisi hiyo wanaotarajia kustaafu mwaka huu walipomtembelea kujifunza mafanikio yake. 
Mmoja wa wastaafu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nisetas Kanje akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda walipomtembelea nyumbani kwake eneo la Zuzu Dodoma kwa lengo la kujifunza Stadi za maaisha pindi watakapostaafu ikiwa ni moja ya shughuli anazofanya baada ya kustaafu

Muonekano wa moja ya mabwawa ya kufugia samaki aina ya sato katika shamba la Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda lililopo Kijiji cha Zuzu Jijini Dodoma ikiwa ni moja ya shughuli anazofanya baada ya kustaafu.




Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda akizungumza na baadhi ya wastaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu walipomtembelea nyambani kwake eneo la Zuzu Jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu juu ya maandalzi ya kustaafu.Ziara hiyo ilifanyiki ikiwa ni sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea 

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda akiwaonesha waastafu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu moja ya Bwawa la kufugia samaki aina ya kambale lililopo katika shamba lake eneo la Zuzu Jijini Dodoma walipomtembelea ikiwa  ni sehemu ya mwendelezo wa mafunzo yaliyotolewa na ofisi hiyo kwa wastafu hao katika kuiadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea.

Muonekano wa sehemu ya shamba la zabibu linalomilikiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda eneo la Zuzu Jijini Dodoma ikiwa ni moja ya shughuli anazofanya baada ya kustaafu. 
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda akiwaonesha baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu mwaka huu ufugaji wa kuku walipomtembelea katika makazi yake eneo la Zuzu Jijini Dodoma ikiwa  ni sehemu ya kujifunza namna ya kufanya ujasilimali watakapostaafu. 
Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akizungumza jambo wakati wa kikao kifupi cha watumishi wa ofisi yake wanaotarajia kustaafu (hawapo pichani) pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda walipomtembelea katika makazi yake eneo la Zuzu Jijini Dodoma. 
 Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda akiwaonesha baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Wazri Mkuu wanaotarajia kustafuu mwaka huu sehemu ya miti ya miembe aliyolima katika shamba lake eneo la Zuzu Dodoma, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu walipomtembelea nyumbani kwake eneo la Zuzu Jijini Dodoma Juni 20,2019.Kushoto kwake ni  Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na.Mwandishi Wetu.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo  Pinda amewaasa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni kudumisha nidhamu katika matumizi ya fedha baada ya kustaafu utumishi wa umma na kujikita katika shughuli za uzalishaji.

Akizungumza katika makazi yake yaliyopo Zuzu Jijini Dodoma  wakati watumishi hao walipomtembelea Juni 20, 2019 kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji katika sekta ya kilimo na mifugo ikiwa ni sehemu ya  maandalizi ya kustaafu pamoja na kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma , Mhe Pinda amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa watumishi wote wanaotarajia kustaafu kujenga utamaduni wa nidhamu katika matumizi ya rasilimali ikiwemo fedha watakazopata kama kiinua mgongo.

"Nidhamu ya maisha baada ya kustaafu ni muhimu sana hivyo niwaase mjitahidi kuacha baadhi ya masuala ambayo mnafanya  kwa sasa kama starehe na mambo yote yanayoendana na kupoteza muda wenu badala yake mjikite katika uzalishaji" Alisisitiza Mhe. Pinda

Aliongezea kuwa  ni vyema watumishi  hao wakajenga utamaduni wa kufanya kazi za uzalishaji na kujikita katika usimamizi wa  miradi ya uzalishaji watakayoanzisha kwa lengo la  kujiongezea kipato na kukuza uchumi .

Pia aliwaasa watumishi hao kuzingatia mawazo kutoka kwa watumishi ambao wameshastaafu na wamefanikiwa  kimaisha baada ya kustaafu.

"Kila mmoja wenu akatekeleze miradi ya kujikwamua kiuchumi kwa kuzingatia mafao atakayopata badala ya kutaka kufanya mambo kwa mashindano bali kila mtu ajikune kulingana na mkono wake unapoweza"

Kwa upande wake Katibu mkuu wa  Ofisi ya Waziri Mkuu  (Bunge na Waziri Mkuu) Bi Maimuna Tarishi amesema kuwa mafunzo yakuwajengea uwezo wa kujiandaa  kustaafu,  yameandaliwa ikiwa ni sehemu ya  maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma.

Aliongeza kuwa watumishi hao wamefarijika kuona shughuli za uzalishaji anazofanya Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda na kuwa ni mfano kwa watumishi wa umma wanaostaafu  na kuanza kujikita katika uzalishaji mali .

Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa mafunzo ya siku 5 kwa watumishi wake wanaotarajia kustaafu ili kuwapa mbinu za kisasa zinazolenga kuwawezesha kuendelea na maisha yao baada ya kustaafu huku wakiendeleza shughuli za uzalishaji  zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku na kuweza kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.