Habari za Punde

BENKI YA DUNIA NA TANZANIA WAWEKA HISTORIA MENEJIMENTI YA MAAFA AFRIKA

 Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali  Jimmy Matamwe (mwenye tai nyekundu), kushoto ni kwake Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi hiyo (Utafiti na Mipango), Bashiru Taratibu, kushoto kwake ni Wawezeshaji  kutoka Benki ya Dunia, Elad Shenfeld, Adam Mc Allister na HugoWesley, wakati  wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji  wa Mpango wa  Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa  taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa , mjini Arusha tarehe 16 Julai, 2019.
 Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na wataalam kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo  wa Utekelezaji wa Mipango ya  menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha
 Mkurugenzi  Msaidizi  (Utafiti na Mipango), Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu Bashiru Taratibu akisisitiza jambo kwa wataalam kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa  zoezi la mezani la kupima uwezo wa wa Utekelezaji wa Mipango
 Mwezeshaji kutoka Benki ya Dunia Adam Mc Allister akisisitiza umuhimu wa Mipango ya Menejimenti ya Maafa kwa   taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa  zoezi la mezani la kupima Utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha, Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
 Mtaalam wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Charles Msangi akieleza jinsi ofisi hiyo inavyoratibu shughuli za maafa wakati wa  zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa  mjini Arusha,
 Baadhi ya washiriki kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa  Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
Mwezeshaji kutoka Benki ya Dunia,  Elad Shenfeld akisisitiza umuhimu wa mipango ya menejimenti ya maafa kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa  zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha, Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
 Kwa mara ya kwanza Barani Afrika na kwa mara ya kwanza katika utendaji wake Benki ya Dunia, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia  Ofisi ya Waziri  Mkuu,  Idara ya Menejimenti ya Maafa, wamefanya zoezi la mezani la  Kupima uwezo utekelezaji  wa Mpango wa  Kujiandaa na kukabili Maafa kwa kutumia maafa ambayo yamepata kutokea kweli hapa nchini, ambapo zoezi hilo limetumia maafa ya   mafuriko mkoani Morogoro, wilayani  Kilosa kwa mwaka 2014 na mwaka 2016. Mazoezi mengine ya mezani ya kujiandaa na kukabli maafa hutumia matukio ya maafa ya kinadharia na hufanyika kabla ya maafa kutokea.

Mtaalam Mwandamizi wa menejimenti ya Maafa, kutoka Benki ya Dunia, Elad Shenfeld, amebainisha mambo matano ambayo yameifanya Benki hiyo kuichagua Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika  kufanya zoezi hilo, kuwa ni Uwajibikaji na uwazi katika kuratibu shughuli za menejimenti ya  maafa unaofanywa na  serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa,  uwepo wa Sheria ya Maafa, ambayo ni  Sheria  ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2015, Mpango wa Taifa wa kujiandaa na Kukabili maafa wa mwaka 2012, Uwezo, Weledi na Uwajibikaji wa watumishi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika menejimenti ya maafa  pamoja na Ushirikiano mzuri wa serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia Tanzania na Kanda ya Afrika katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini.

Akiongea mara baada ya kufunga zoezi hilo mjini Arusha, tarehe 16, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amebainisha kuwa nchi nyingi barani Afrika ikiwemo Tanzania zimekuwa zikifanya  mazoezi ya kujiandaa na kukabili maafa kwa kutumia nadharia za maafa yanoyoweza kutokea, lakini zoezi hilo  ni tofauti kwani limejikita kwa maafa ambayo yamewahi kutokea kweli  hapa nchini.

“Zoezi hili  ambalo limeangalia maafa ya mafuriko yaliyotokea, Kilosa kwa mwaka 2014 na 2016,  litatusaidia kuimarisha mifumo yetu serikalini ya kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko na majanga mengine kwani tumejua ni wapi hatukufanya vizuri na namna gani ya kuboresha mifumo yetu,  lakini pia zoezi hili litawajengea uwezo waratibu wa maafa serikalini na wataalam kutoka katika mashirika yasiyokuwa ya serikali katika kushirikiana na serikali katika kujiandaa na kukabili maafa yatapotokea” Alisema Matamwe.

Aidha, washiriki wa zoezi hilo waliweza kutoa uzoefu wao katika kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko ambayo yalitokea wilayani Kilosa  kwa mwaka 2014 na 2016. Washiriki hao kwa nyakati tofauti walibainisha kuwa wamejifunza kutoka mafuriko ya Kilosa kuwa ipo haja ya kila Serikali za mitaa na Taasisi za serikali pamoja na wadau wa menejimenti ya maafa kutenga bajeti kwa ajili ya masuala ya usimamizi wa shughuli za maafa.

Zoezi hilo lililofanyika kwa muda wa siku mbili tarehe 15 hadi 16, Julai, 2019,  liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa shughuli za maafa kutoka serikalini na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali, limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa,  kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.