Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza nan wananchi kwenye mkutano wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kasamwa mkoani Geita ambapo amewashauri wakulima wasiuze pamba yao kwa walanguzi ambao wamekuwa wakinunua kwa bei ndogo.
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Geita, Bw. Barnabas Mapande akizungumza na wananchi wa Kata ya Kasamwa kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza nao.
Diwani wa Kata ya Kanyala, Mhe. Logaloga akizungumza na wananchi kwa jinsi anavyoshirikiana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Geita mjini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu akiwatambulisha Makatibu wake kwa wananchi wa Kata ya Kasamwa mara baada ya kuzungumza na wananchi hao mamabp mbalimbali ikiwemo bei ya pamba, ufumbuzi wa suala la maji na nishati ya umeme
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na watumishi wa Umma mara baada ya mkutano wa hadhara kufunguliwa katia kata ya Kaswama mkoani Geita.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kasamwa waliokusanyika katika eneo la mkutano kwa ajili ya kumpokea Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewashauri Wakulima wa zao la pamba wawe wavumilivu badala ya kuuza pamba hiyo kwa walanguzi kwa bei ya chini huku Serikali ikiendelea kuwatafutia soko zuri.
Amesema Serikali ilishaahidi kuwa kama pamba hiyo haitanunuliwa kwa bei elekezi ya kilo moja kwa shilingi 800 hadi mwezi Agosti mwaka huu basi Serikali itainunua pamba hiyo ili kuwafidia wakulima hao.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Wafanyabiashara wengi kushindwa kununua kwa bei hiyo kutokana bei ya soko la pamba duniani kuporoka.
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika eneo la Kasamwa mkoani Geita, Mhe.Kanyasu amesema wafanyabiashara wameshindwa kukopa pesa benki kwa ajili ya kuinunua pamba hiyo kutokana na kukosekana kwa soko la kuiuza.
Mhe.Kanyasu amesema kufuatia hali hiyo baadhi ya wakulima wamekuwa wakiiuza pamba hiyo kwa shilingi 500 kwa kilo moja kwa walanguzi hali inayowadidimiza kiuchumi.
Ametaja mikakati ambayo tayari Serikali imeshaichukua ikiwemo kuzungumza na Serikali ya Vietnam ambao tayari wameonesha nia ya kununua pamba hiyo kwa Wakulima.
Aidha, Mhe Kanyasu amewaeleza Wakulima hao kuwa Waziri wa Kilimo anatambua tatizo hilo na ameahidi kutembelea mkoa huo kwa ajili ya kuzungumza na Wakulima hao.
Naye Juma Kaludushi ambaye ni mkulima wa zao pamba amesema wakulima walio wengi akiwemo na yeye wamekuwa wakiuza pamba hiyo kwa walanguzi kwa bei ya chini kwa hofu kuwa pamba hiyo itaharibika mikononi mwao.
"Pamba ipo majumbani mwetu muda unakwenda bora tuuze tu kwa Walanguzi ili isiharibike kuliko tukapata hasara kabisa" Amesema Mkulima huyo.
Kwa upande wake, Ester Nalamo, ambaye ni Mkulima wa pamba amesema amelazimika kuuza pamba kwa bei ya chini ili aweze kuwalipia ada watoto wake kwa vile yeye hana chanzo kingine cha mapato zaidi ya kuuza pamba.
No comments:
Post a Comment