Habari za Punde

Waandishi wa Habari Zanzibar Waadhimisha Miako 70 ya Taifa la China


Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (kulia)akimkabidhi zawadi ya Kitabu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu akitoa hotuba katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dk,Juma Mohamed Salum akitoa hotuba katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (katikati)akiwa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum wakichukua chakula katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Waandishi wa Habari wakichukua chakula  katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (katikati)akiwa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum kushoto yake katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari mbalimbali katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.

Na. Ali Issa  - Maelezo  
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imekuwa mshirika mkubwa wa kimaendeleo kwa Zanzibar katika sekta mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii.
Hayo yamesemwa huko Hoteli ya Verde na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dkt. Juma Muhammed Salum katika sherehe za miaka 70 ya kuundwa kwa Jamuhuri ya Watu wa China na miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya China na Tanzania.
Amesema China ilikua ni nchi ya kwanza kuiunga mkono Zanzibar mara baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na ushirikiano huo umekuwa ukiendelea hadi hivi sasa.
Aliongeza kusema kuwa China imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Zanzibar na kuiletea maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, kilimo, utamaduni na michezo.
Alikumbusha juu ya ujenzi wa hospitali ya Abdalla Mzee Pemba, ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Amanai na Mao tse Tung na kusaidia kuleta madaktari na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali kuu ya Mnazimmoja na ile ya Mkoani.
Aidha alisema wameweza kusaidia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar na miundo mbinu ya Barabara na huduma za mawasiliano kwa kuweka taa katika barabarani mbali mbali za Zanzibar.
Alisema uhusiano uliopo kati ya China na Tanzanzia ni wa kipekee kwani Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alikuwa kiongozi pekee alieweza kukutana na Baba wa Taifa la China Marehemu Mao mjini Beijing mara nyingi zaidi kuliko kiongozi mwengine yoyote katika uhai wake.
Aidha Mkurugenzi huyo alilieleza kuwa China imekuwa ikitoa elimu kwa vijana wa Zanzibar katika fani tofauti na imekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi  Zanzibar.

Nae Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu alisema kuwa Nchi yake imekuwa rafiki wa kweli na Tanzania na imekuwa mstari wa mbele kuongeza misaada yake kwa Taifa hilo na Afrika kwa Ujumla .
Aliongeza kuwa China inaendeleza juhudi za upatikanaji wa huduma za maji safi na salama mijini na vijijini kwa kuchimba visima vipya katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na kujenga matangi mapya ya kuhifadhia maji Saateni na Kilimani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.