Habari za Punde

WAZIRI JENISTA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye  Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na waombolezaji wakati alipowaongoza katika Ibada na kuaga mwili wa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Richard Kalinga, nyumbani kwa marehemu jijini Dodoma, Julai  22, 2019. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maadhimisho, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mohammed  Kiganja
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akitoa pole kwa familia ya mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu  Richard Kalinga, baada ya kuwaongoza waombolezaji katika Ibada ya kumwombea marehemu na kutoa heshima za mwisho, nyumbani kwa marehemu jijini Dodoma Julai 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.