Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kutimua Vumbi Mwezi Ujao kwa Mchezo wa Ngao ya Hisani Kati ya KMKM na Malindi Utakaofanyika Uwanja wa Amaan 1-9-2019.

Na.Mwajuma Juma.
MCHEZO  wa Ngao ya Hisani kuashiria kufunguwa ligi  Kuu ya Zanzibar inatarajiwa kuanza Septemba mosi mwaka huu.

Mchezo huo wa utawakutanisha KMKM ambao Ni mabingwa wa Zanzibar msimu wa 2018/2019 na Malindi ambao ni Makamo bingwa, utapigwa katika uwanja wa Amaan Mjini hapa majira ya saa 10:00 za jioni.

Akizungumzia mchezo huo Mjumbe wa Kamati ya mashindano ya ZFF Hawa Abdalla Ali alisema kuwa mchezo huo wa ngao ya hisani utakuwa Ni tofauti na ilivyozoeleka .

Alisema kuwa kabla ya kuchezwa mchezo huo kutaanza burudani na baadae saa 8:00 mchana kutakuwa na mchezo wa ngao ya hisani kwa timu ndogo Kati ya KMKM na Malindi.

Aidha alisema kuwa katika burudani kutakuwa na msanii kutoka Tanzania bara ambae atakuwa ni balozi wa mwana FA kwa upande wa Tanzania bara pamoja na.msanii mwengine kutoka visiwani ambae watamtangaza hapo baadae.

Alifahamisha kwamba wameamuwa kuweka burudani mbali mbali katika uzinduzi huo ili kuashiria kuanza kwa Msimu huo mpya wa ligi na kuona kwa namna gani wanawavutia mashabiki.

Timu zinazoshiriki ligi hiyo kwa Msimu wa 2019/2020 ni KMKM, Malindi, Zimamoto, Polisi, KVZ, Mafunzo, Jamhuri, Jang'ombe Boy's, Mwenge, Selem View, Chuoni, Chipkizi, Kipanga na Machomane.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.