Habari za Punde

Wadau wa Nafaka Wakutana Jijini Dar es Salaam Kujadili Fursa.


Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akihutubia mkutano wa Wafanyabiashara wa Nafaka wa Ndani na Nje ya Nchi uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MKUTANO wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi umefunguliwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, 2019.
Mkutano huo ambao umewajumuisha wasindikaji, wasafirishaji na wamiliki wa maghala ya nafaka Lengo lake ni kuangalia fursa zilizopo kwenye tasnia ya nafaka na jinsi ya kuzifikia ikiwa ni pamoja na masoko.
Akizungumza na washiriki wa mkutano huo uliowakutanisha  wadau kutoka mikoa mbalimbali  nchini, Mhe. Hasunga ambaye alifuatana na Manaibu wake, Mhe. Husein Bashe, na Mhe. Omary Mgumba alisema mkutano huo utatoa fursa kwa wajumbe kuelimishwa kuhusu fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika, uwezo wa Tanzania kuzalisha na nafasi ya wafanyabiashara kushiriki kikamilifu lakini pia washiriki watapata fursa ya kujifunza athari za upotevu wa mazao ya nafaka baada yamavuno na mkakati wa serikali kudhibidi hali hiyo.
“Kitaalamu wanasema utafiti uliofanyika Tanzania na  nchi nyingi za Kusini asilimia 40 ya mazao yote yakiwemo ya nafaka yanapotea baada ya mavuno kwa kuharibika na matatizo mengine, hii haikubaliki mkulima amewekeza, amevuna halavu mazao yake yanaharibika, lazima tuwe na mkakati wa kuzuia hali hii.” Alitoa hakikisho Mhe. Waziri Hasunga na kuongeza.
Kulingana na uzalishaji uliopo, nafaka nyingi kama mahindi mtama na nafaka nyingine huhifadhiwa katika kiwango kisichoridhisha hali hii huchangia kupoteza ubora wa nafaka na hatimaye huchangia kuzorota kwa ustawi wa afya zetu, alifafanua zaidi Mheshimiwa Waziri.

Alisema Agosti 1, mwaka huu kwenye sherehe za Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganow a Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua mkakati wa namna ya kupambana na kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno.
Katika utafiti wake ilioufanya hivi karibuni Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya Mradi wa Rapid Response Implementation Support to the Ministry of Agriculture and Agriculture Sector Lead Ministry (RARIS) unaofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation umebaini kuwa hali ya maghala mengi ya watu binafsi hayatoi taarifa serikalini na hii ni kutokana na mfumo wa sasa wa maghala.

Akitoa mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses), Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt.Hoseana Lunogelo alisema ESRF ilifanya utafiti wa hali (status) ya maghala nchini na kubaini kuwa maghala ya watu binafsi hayalazimiki kisheria kutoa taarifa serikalini kuhusu nini kimehifadhiwa na kiasi gani cha nafaka kilichohifadhiwa ndani ya maghala hayo na hali hii serikali inategemea tu maghala ya Serikali yaani (Public Storage Facilities ) kupitia Werehouse Reseat Regulatory Board ili kujua takwimu za hali ya chakula nchini.
“Kwa sasa kuna maghala 3,430 yaliyopo kati ya hayo ni 185 tu ndiyo kuna uhakika wa kupata tawimu endapo zitahitajika lakini yaliyosalia huwezi kupata takwimu hizo kwa sababu hakuna sheria inayowalazimisha kufanya hivyo.” Alifafanua Dkt. Lunogelo.

Alisema hii ni changamoto kubwa, kama serikali inapata taarifa kutoka kwenye maghala machache sana nchini na yale mengi haipati taarifa zake, maana yake Serikali haiwezi kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na upatikanaji wa chakula nchini na hiyo ina athari mbaya kwenye usalama wa chakula na pia ina athari mbaya pia kwenye biashara.” Alsiema Dkt.Lunogelo.
 Wadau wa mazao ya nafaka, wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Japhate Hasunga wakati akihutubia mkutano wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi  kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam 
 Mhe.  Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akihutubia mkutano huo.
 Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
 Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
 Bi. Margareth Nzuki (katikati), akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF akifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na Dkt. Bunogelo kuhusu utafiti ambao ulifanywa na Taasisi hiyo kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).

 Mkuurgenzi Mtednaji wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw.Japhet Justine akipiga makofi wakati mkutano huo ukiendelea.
 Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
  Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
 Bi.Margareth Nzuki (kushoto), kutoka ESRF akibadilishana mawazo na Bi. Vumilia L. Zikankuba kutoka Wizara ya Kilimo wakati wa mkutano huo.
 Mshiriki akitoa maoni yake.
 Oswald Mashindani (kushoto), kutoka ESRF akizunhumza jambo mbele ya Katibu Mkuu (mstaafu) Wizxara ya Fedha, Bw. Paniel Lyimo (katikati) wakati wa mkutano huo.
 Mhe. Hadsunga (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na manaibu waziri makatibu wakuu na Mwenyekiti wa TPSF.
 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.