Habari za Punde

ZAIDI YA BILIONI SITA ZATUMIKA KULETA MAENDELEO KATA YA MAPANDA.

Diwani wa kata Mapanda Obadia Kalenge akielezea jinsi gani walivyotumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu,afya na utamaduni

Na. Fredy Mgunda - Iringa.
Zaidi ya bilioni sita zimetumika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu,afya na utamaduni katika kata ya Mapanda iliyopo katika jimbo la Mufindi kaskazini ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.

Akizungumza na blog hii diwani wa kata hiyo Obadia Kalenge alisema kuwa katika sekta ya elimu wamefanikiwa kujenga majengo mapya katika shule mbalimbali zilizopo katika kata hiyo kwaushirkiano wa serikali,wananchi na wadau mablimbali wa maendeleo waliopo katika kata hiyo.

“Nguvu ya wananchi ilikuwa ni mchanga na mawe tu,mfano shule ya Kihansi pekee yake ina miradi inayogharimu kiasi cha shilingi milioni mia sita themanini na nane na laki tano hivyo nina shule saba na jumla ya shilingi milioni mia nane na sitini zimetumika kuleta maendeleo kwenye elimu katika kata yangu ya Mapanda” alisema Kalenge

Kalenge alisema kuwa katika sekta ya afya amefanikisha uwepo wa CTC kuwepo kwenye kata hiyo na kuanza kujenga jingo la wodi ya akina mama na watoto na kuendelea na ujenzi wa kituo cha afya na kata ya hiyo inavijiji vitano hivyo kila kijiji kina zahanati ambayo imekuwa ikasidia kuta huduma ya afya kwa wananchi wa kata hiyo.

“Mwaka jana wakati wa bajeti nilijenga hoja kwenye baraza la madiwani kwa kuomba kujengewa kituo cha afya ambapo halmashauri walinikubaria ombi langu na kuhakikisha mwisho mwa 2019 kituo hicho cha afya kinakuwa kimeanza kufanya kazi” alisema Kalenge
 
Kila zahanati kuna mganga na nesi  na kuongeza kila zahanati zilizopo katika kata hiyo kuna pikipiki ambazo zimekuwa zikisaidia katika usafiri  wa hapa na pale kutokana na mazingira ya kata hiyo hivyo usafiri wa pikpiki umekuwa ukirahisisha utendaji kazi kwa watumishi wa afya wa kata hiyo.

Aidha Kalenge alisema kuwa swala la barabara limekuwa changamoto kubwa kutokana na barabara hizo kuharibika mara kwa mara na zinatumia gharama kubwa kukarabati miundombinu hiyo laki kuna barabara ya kutoka Chogo hadi Isipi kwa mara ya kwanza ndio imetengenezwa kwa mara ya kwanza toka kuumbwa kwa dunia.

“Ili kurahisisha maendeleo lazima kuwe na miundombinu bora hivyo nimepigana navyoweza kwa ushirikiano mkubwa na mbunge wa jimbola Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa tumefanikiwa kutatua kero hiyo kwa kiasi chake” alisema Kalenge

Kalenge alisema kuwa tatizo la maji linaelekea kutatuliwa kutokana najuhudi zinazofanywa kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanapata maji kwa kutumia mamilioni ya fedha kutoka kwa wadau na serekali ambapo wananchi wameshachanga na serikali tayari imeleta wataalamu kwa ajili ya kutatua kero hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.