Habari za Punde

ESRF Yazindua Program ya Kuwajengea Uwezo Watanzania.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi, Mary Maganga, akitoa hotuba yake wakati akizundua Programu ya Impact Evaluation Laboratory kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii Nchini (ESRF) jijini Dar es Salaam, Septemba 23, 2019.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SERIKALI imeipongeza Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii Nchini (ESRF) kwa kuelewa agenda ya taifa ya kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kuja na mkakati wenye manufaa wa kutoa mafunzo ya tafiti za aina mbalimbali juu ya upimaji wa matokeo mwishoni mwa mradi (Impact Evaluation Laboratory) kwa watumishi wa Umma na wale wa Mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizindua Program ya miaka miwili kuwajengea uwezo Watanzania katika kufanya utafiti wa aina mbalimbali unaohusiana na upimaji wa matokeo (Impact Evaluation Laboratory) kwenye ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii Nchini (ESRF) jijini Dar es Salaam Septemba 23, 2019, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi, Mary Maganga amesema, mafunzo hayo yatasaidia sana wataalamu hapa nchini kutoka Serikalini sambamba na wataalamu kutoka taasisi binafsi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs).
Alisema Serikali ya Awamau ya Tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, imetambua umuhimu wa kuwaletea maendeleo wananchi ambapo tangu iingie madarakani imekuwa ikitekeelza miradi yenye matokeo chanya kwa ustawi wa wananchi.
“Hii imekuwa ikisisitizwa na Rais mara kwa mara na kila mwaka kwa miaka mitatu mfululizo Serikali imekuwa ikitenga kiasi cha asilimia 37 ya bajeti yake kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.” Alifafanua Bi. Mary.
Alisema kwa sasa Serikali kuu inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ya miundombinu kama vile ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge (SGR), Mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere wa Megawati 2115 (JNHPP), Barabara, Madaraja na Miradi mingine mingi ambayo inaendelea kutekelezwa.
Hali kadhalika Bi. Mary alisema katika Serikali za Mitaa miradi ya kijamii katika maeneo ya afya, elimu na mingine ya kimkakati nayo pia inatekelezwa. Aidha Mashirika ya umma, binafsi, NGOs na wadau wa maendeleo, pia wanasaidia jitihada hizi za serikali za kuinua ustawi wa wananchi.
“Ili kuratibu miradi hii ya maendeleo kunahitajika timu ya wataalamu kama ninyi ambao mtakuwa na uwezo wa kufanya tafiti za kisayansi za matokeo ya miradi hii baada ya kukamilika.” Alisema Bi. Mary.
Profesa Fortunata Makene – Mkuu wa idara ya Utafiti na Machapisho (ESRF) akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii Nchini (ESRF), Dkt.Tausi Mbaga Kida, alisema kwa takriban miaka minne mfululizo ESRF imekuwa ikijielekeza kuwajengea uwezo wataalamu wa hapa nchini kuhusu upimaji wa matokeo mwishoni mwa mradi (impact evaluation)
“Mnamo mwaka 2015 Taasisi ilitangaza na kuendesha mafunzo ya wiki moja kuhusu upimaji wa matokeo ambapo  wanafunzi 17, na tulirudia kutoa mafunzo kama haya mwaka 2016, 2017.” Alibainisha Profesa Makene.
Mwaka jana 2018 ESRF ilipata ufadhili kutoka Taasisi ya William na Flora  Hewlett na kupitia ufadhili huo ESRF ilitoa mafunzo ya wiki tatu kwa wanafunzi 40 ambao ni pamoja na watafiti wa Sera na Mameneja Miradi lakini pia tulitoa mafunzo ya wiki moja kwa watumishi 20 wa Serikali.
Kutokana na mafanikio hayo ya mwaka 2018, mwaka huu wa 2019 ESRF ilipokea ufadhili wa pili  ili kuanzisha Impact Evaluation Laboratory.
“Impact Evaluation Laboratory ni mradi wa miaka miwili kujengea uwezo Watanzania katika kufanya utafiti wa aina mbalimbali unaohusiana na upimaji wa matokeo (Impact Evaluation) ambao umeandaliwa na unatekelezwa na ESRF.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi, Mary Maganga, akitoa hotuba yake wakati akizundua Programu ya Impact Evaluation Laboratory kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii Nchini (ESRF) jijini Dar es Salaam, Septemba 23, 2019. Katikati ni Profesa Fortunata Makene na Mkufunzi wa mafunzo hayo Bw.Costantine Manda
 Mkuu wa Idara ya Mikakati ya Utafiti na Machapisho (ESRP), Profesa Fortunata Makene, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Tausi Mbaga Kida, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Mkuu wa Idara ya Mikakati ya Utafiti na Machapisho (ESRP), Profesa Fortunata Makene, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Tausi Mbaga Kida, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mratibu wa mafunzo, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya uwezeshaji na maendeleo ESRF, Bw.Danford Songo, akieleza nia ya mafunzo hayo.
  Mkufunzi wa mafunzo hayo, ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa Programu ya Impact Evaluation Laboratory, Bw.Costantine Manda, akitoa "somo"
 Mkufunzi wa mafunzo hayo, Bw.Costantine Manda, akitoa mafunzo hayo.

 Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo 
 Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo 

 Mshiriki akizungumza.
 Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo 
 Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo 
 Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo 
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi, Mary Maganga (kulia), akizungumza jambo na Mwezeshaji (Trainer) ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa Programu ya Ipmact Evaluation Laboratory, Bw. Costantine Manda
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi, Mary Maganga (kulia), akisalimiana na mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Rais, Bw. Joseph Mwacha, huku mratibu wa mafunzo hayo ambaye ni Mkuu wa Idara ya uwezeshaji na maendeleo ESRF, Bw.Danford Songo akishuhudia.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi, Mary Maganga (kulia), akifurahia jambo na Mkuu wa Idara ya uwezeshaji na maendeleo ESRF, Bw.Danford Songo.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi, Mary Maganga (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Mikakati ya Utafiti na Machapisho (SRP), wa Taasisi hiyo, Profesa Fortunata Makene
Mgeni rasmi katika Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.