Habari za Punde

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi Ajumuika Katika Chakula Maalum cha Mchana na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbaramo.

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini  Mhe. Mohamed Raza akisisitiza azma yake ya kuendelea kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum wakati akikabidhi vifaa kwa wanafunzi wa skuli ya msingi ya Mbaramo iliopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga
Mkuu wa wilaya ya Muheza Injinia Mwanaasha Tumbo akiwalezea wananchi wa wilaya ya Muheza mafanikio ya serikali ya awamu ya tano katika kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalum kwa wilaya ya Muheza katika mkutano wa makabidhiano ya vifaa vya Bweni la wanafunzi vilivyotolewa na Muwakilishi wa jimbo la Uzini Mhe. Mohamed Raza.
Mama Asha Suleiman Iddi akiwa pamoja na viongozi wa serikali wa wilaya ya Muheza pamoja na viongozi Chama cha mapinduzi wakishirikiana pamoja katika kuwafariji watoto wenye mahitaji maalum mara baada ya kula nao chakula cha mchana.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwafariji watoto wenye mahitaji maalum wa skuli ya msingi Mbaramo iliopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga mara baada ya kula nao pamoja chakula cha mchana.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwafariji watoto wenye mahitaji maalum wa skuli ya msingi Mbaramo iliopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga mara baada ya kula nao pamoja chakula cha mchana.
Picha na OMPR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.