Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiingia katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar katika hafla ya kuwaapisha Washauri katika sekata mbali mbali baada ya kuwateuwa rasmi katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Abdalla Rashid Abdulla kuwa Mshauri wa Rais Mambo ya Siasa katika iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo Bw.Ali Mzee Ali baada ya kuapisha kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya Historia na Mambo ya Kale katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid,Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassaan Said pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika hafla ya kuapishwa washauri akiwemo Mshauri wa Rais Siasa Bw.Abdalla Rashid Abdulla na Bw.Ali Mzee Ali Mshauri wa Historia na Mambo ya Kale katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo
Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa washauri akiwemo Mshauri wa Rais Siasa Bw.Abdalla Rashid Abdulla na Bw.Ali Mzee Ali Mshauri wa Historia na Mambo ya Kale katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali na Mshauri wa Rais Mhe.Chimbeni Kheri Chimbeni
Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment