RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali
Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China Mhe.Xi
Jinping pamoja na wananchi wa Taifa hilo kwa kuadhimisha miaka 70 tangu kuundwa kwake.
Katika salamu zake alizotuma kwa Rais Xi Jinping, Dk. Shein
amesema kwa niaba ya wananchi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anatoa
pongezi za dhati kwa Taifa hilo kwa mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii
yaliofikiwa, katika kipindi hicho.
Amesema Zanzibar inajivunia urafiki na uhusiano mzuri wa
kihistoria uliopo kati yake na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China, ikiwa ni
matokeo yatokanayo na uongozi bora na uliotukuka kutoka kwa mwasisi wa Taifa
hilo Mwenyekiti Mao Zedong.
Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaunga mkono
juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Taifa hilo , ikiwa ni hatua ya kuunga mkono
mawazo ya muasisi wake Mweyekiti Mao.
Rais Dk. Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza
uhusiano wa kindugu na ushirikano uliopo kati yake na Jamuhuri ya Watu wa China,
kwa maslahi ya wananchi wake.
Aidha, Dk. Shein
ametumia fursa hiyo kumtakia afya njema na maisha yenye furaha Rais Xi
Jinping pamoja na wananchi wote wa Taifa
hilo.
Abdi
Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822
E-mail:
abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment