Habari za Punde

UVCCM Iringa Wampongeza Diwani Nguvu Chengula Kwa Mchango wa Kimaendeleo wa Umoja huo.

Diwani Nguvu Chengula akiongea kwenye mkutano wa kusikiliza kero kwa madereva bajaji na madereva boda boda wa Manispaa ya Iringa wakati wa kusikiliza kero zao mbele ya mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa.

Na.Fredy Mgunda -Iringa.
Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa kimempongeza diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Edward Chengula kwa mchango anaoutoa wa kusaidia kutatua baadhi ya changamoto ambazo wamekuwa wanakumbana nazo.

Akizungumza kwenye mapokezi ya mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi mara baada ya kumaliza majukumu ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa na kurudi kwenye majukumu ya kichama mkoani Iringa,katibu wa UVCCM manispaa ya Iringa  Sai Samba alisema kuwa diwani Nguvu Chengula amekuwa akitoa misaada mbalimbali katika umoja huo.

“Ndugu mwenyekiti unaona vijana hawa wa green guard wamependeza kwa sare safi,hivi zote ni juhudi za diwani huyu ambaye alijitolea kitambaa ambacho kilisaidia kushona sare hizi japo bado tunauhitaji wa sare hizo na bado amekuwa msaada wa kwenye mambo mengi ya umoja wetu” alisema Samba

Samba aliongezea kuwa UVCCM manispaa ya Iringa bado wanauhitaji mkubwa wa sare za green guard hivyo wanaomba msaada kwa diwani huyo kuwawezesha kupata sare nyingine ambazo zitawawezesha vijana wote wa green guard kuwa na sare ambazo zitatumika kwenye matukio mbalimbali ya chama.

“Mheshimiwa diwani ikikupendeza tunaomba tuongezee kitambaa kingine ili tushone sare ambazo zitakuwa zimetatua tatizo hilo licha kuwa bado umoja huo unachangamoto nyingi” alisema Samba

Naye mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya ya Iringa Vijijini Makalah Mapesa alisema kuwa moja kati ya madiwani wa Iringa Mjini ambaye amekuwa na msaada katika wilaya hiyo ndi diwani Nguvu Chengula ambaye amekuwa akisaidia mambo mengi

"kiukweli mimi naomba nimpongeze diwani Nguvu Chengula kwa mchango wake ambao amekuwa akiutoa wilaya ya Iringa vijijini kimaendeleo" alisema Mapesa

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa (UVCCM) Kenani Kihongosi alimpongeza diwani huyo kwa mchango wake kwa kuwa amepokea salamu kutoka kwa viongozi wake wa chi kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha anatatua changamoto za umoja huo.

“Kama kweli unatoa msaaada huo kwa roho nzuri mimi kama mwenyekiti nakupongeza sana ila kama unatoa kwa lengo la kitu hapo baadae basi jiandae kukatwa jina pindi utakapoanza harakati zako hivyo niwakumbushe viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kuacha tabia ya kutoa Rushwa kwa vijana” alisema Kihongosi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.