Habari za Punde

Wazazi mkoani Mwanza watakiwa kuwapeleka watoto kupata chanjo

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano kwenye Vituo vya Afya kupata chanjo bure hidi ya magonjwa ya Surua, Rubella na Polio kuanzia tarehe 17-21 Oktoba 2019.

Kwa Mkoa Mwanza, zaidi ya watoto laki sita (watoto 637,579) wanatarajiwa kupewa chanjo ya Rubella na Polio huku watakaopewa chanjo ya Surua wakitarajiwa kuwa zaidi ya elfu sitini (watoto 266,140) hivyo kufanya jumla ya watoto wanaotarajiwa kuchanjwa kuwa laki tisa elfu tatu  mia saba kumi na tisa (watoto 903,719). 
Kitaifa uzinduzi wa zoezi hilo umefanyika mkoani Morogoro, Oktoba 17, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo dhidi ya Surua, Rubella na Polio.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akitoa salamu za Wizara kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo mkoani Mwanza.
Tazama Video hapa vhini

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.