Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli
Bw. Eric Hamissi akimpa maelezo Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi
hatua iliyofikiwa ikiwemo vifaa ambavyo vimeshawasili nchini mpaka sasa kwa
ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria ambapo Serikali imeweka Kiasi cha
Shilingi Bilioni 89 katika mradi huu.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari -
MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi jana (Oktoba 31)
alitembelea mradi wa ujenzi wa meli ya
kisasa ambayo ni meli kubwa kuliko zote katika Ukanda wa Afrika Mashariki
pamoja na ujenzi wa chelezo kwa ajili ya matengenezo na marekebisho ya meli
mbalimbali ikiwa ni uwekezaji unaofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Akiwa katika eneo hilo, Dkt. Abbasi alisema kuwa ujenzi wa meli mpya ni ahadi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 23
iliyopita, ambayo imetekelezwa katika
kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais . Dkt Magufuli.
Aidha, Dkt. Abbasi aliongeza kuwa
ujenzi wa meli mpya itakayokuwa na uwezo
wa kubeba abiria 1, 200 umefikia
asilimia 33 ya ujenzi na utakamilika mapema mwaka 2021, ambapo Serikali
imewekeza zaidi ya TZS Bilioni 150, kwenye mradi ya meli pamoja na ujenzi wa
chelezo.
Aidha, Dkt. Abbasi alishuhudia
ukarabati unaoendelea katika meli ya MV. Victoria, ambayo baada ya kukamilika
itasaidia kutoa huduma bora za usafiri
kwenye eneo la Ziwa Victoria.
Vilevile, akiwa ziarani hapo Dkt. Abbasi alisema kuwa ipo miradi mingi kwenye
eneo la Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika, inatakayo gharimu zaidi ya TZS Bilioni 300.
Aliongeza kuwa hivi karibuni,
Serikali itasaini makubaliano ya utekelezaji
wa miradi ya ujenzi wa meli katika eneo la Ziwa Tanganyika na uundaji
wa meli 3 mpya na za kisasa katika eneo
la Ziwa Nyasa.
Akitaja, meli zilizokamilika
kutokana na utekelezaji wa ahadi za Serikali hadi sasa kuwa ni meli za mbili za
mizigo za MV. Ruvuma, na meli kubwa ya
kisasa ya abiria ya MV. Mbeya II na ambayo tayari imeanza kazi.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Huduma za Meli, Eric Hamissi,
alisema kuwa ujenzi wa meli hiyo
mpya unaendelea vizuri, na Septemba 30, mwaka huu vifaa mbalimbali kwa ajili ya
ujenzi wa vilianza kuletwa na sasa kazi ya uunganishwaji wa vyuma imeshaanza.
Aliongeza kuwa, ujenzi wa chelezo
umefikia 53%, na ifikapo Machi mwakani chelezo itanza kutumika kwa ajili ya
ujenzi wa meli mpya.
Aidha, Bw. Hamissi alisema
anaishukuru Serikali kwa ujenzi miradi hii
miwili pamoja na ya ukarabariti
wa MV. Butiama na MV. Victoria inayoendelea kwani itaigharimu
Serikali TZS Bilioni 150, na hadi sasa Serikali imeshatoa TZS Bilioni 70.8,
sawa na 47% ya miradi yote minne.
Bw. Hamissi, aliongeza kuwa miradi hii imesaidia kukuza
uchumi wa Mwanza kwa kutoa ajira zaidi ya watu 1,000 pamoja utumiaji wa
malighafi na watoa huduma, hali inayosaidia kuboresha maisha ya wananchi.
Alifafanua kuwa, huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na
Serikali ambao haujawahi kutokea tangu
Uhuru na ni mapinduzi katika usafiri wa njia ya maji kwa kutekeleza
miradi mikubwa minne kwa wakati mmoja, na kuwa awali meli nyingi zilijengwa kwa
msaada mfano MV. Sangara.
Naye, Li Yonjee, Mtaalamu wa Meli
kutoka Korea Kusini, alisema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapa fursa
ya kushiriki katika uundaji wa meli mpya ya kisasa, watatumia ujuzi wao wa uundaji wa meli waliofanya
katika nchi za Korea ya Kusini, China na
Japan, zikiwa ndio nchi kubwa za uundaji
wa meli duniani, katika kuunda meli mpya
ya Tanzania.
Vilevile, Bw. Li alisema kuwa wanaahidi kutimiza
matarajio ya Serikali na watanzania kwa ujumla kwa kuunda meli hiyo kwa mafanikio, pamoja kuikamilisha kwa wakati.
Aidha, Bhoke Siguta mwanamke
anayefanyakazi ya kuchomelea vyuma katika mradi wa uundaji wa meli mpya,
alisema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutekeleza miradi mbalimbali
inayogusa maisha ya watanzania, ikiwemo
kutoa ajira.
Bi. Siguta alisisitiza kuwa, kupitia
mradi huu wa uundaji wa meli mpya ameweza kupata ajira, inayompatia kipato cha kumsaidia kutunza
familia yake.
Pia,
ameshauri wanawake kujishughulisha na kazi za uchomeleaji vyuma, kwani ni kazi nzuri na zitawajengea uwezo
zaidi wa kujiamini pamoja na kukuza kipato.
Awali, Dkt. Abbasi alikutana na kufanya mazungumzo
na uongozi wa Kampuni ya Huduma za Meli kuhusu mikakati na maboresho ya kampuni
hiyo.
Meneja Mradi wa Chelezo na Ukarabati wa
Meli za MV. Victoria na MV Butiama Mhandisi Abel Gwanafyo akimpa maelezo Msemaji
Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi
wa Chelezo ambayo ni sehemu kubwa itakayokuwa inapaki meli kwa ajili ya matengenezo
na marekebisho mbalimbali, Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za
Meli Bw. Eric Hamissi
Baadhi ya Mafundi wakiendelea na zoezi la
uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria
itakayofanya kazi katika ziwa victoria.
Baadhi ya Mafundi wakiendelea na zoezi la
uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya kubwa ya abiria
itakayofanya kazi katika ziwa victoria.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi
akiwa katika picha ya pamoja na wakandarasi wanaojenga meli mpya na wafanyakazi
wa Kampuni ya Huduma za Meli alipotembelea eneo hilo ili kujionea hatua
iliyofikiwa ya ujenzi wa meli hiyo itakayofanya kazi katika ziwa victoria.
Muonekano wa Chelezo inayojengwa na Kampuni ya Huduma za Meli ambayo ni sehemu kubwa itakayokuwa inapaki
meli kwa ajili ya matengenezo na marekebisho mbalimbali ambayo imefikia
asilimia 53 ya ujenzi na itaanza kutumika mwezi Machi 2020
No comments:
Post a Comment